“Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha ongezeko la vyombo vya habari mtandaoni haliathiri maadili na utamaduni wa Taifa letu” – Mhe. Toufiq Salim Turky, Mbunge wa Jimbo la Mpendae
“Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kutoa leseni za vyombo vya habari na waandaaji wa maudhui mitandaoni kwa maombi yanayokidhi vigezo vilivyowekwa ili kupanua wigo wa kutoa habari nchini kwa kuzingatia Sheria na kanuni za utangazaji. Hadi kufikia mwezi Machi 2025, leseni 206 za Television na Redio za Mtandaoni zimetolewa” – Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma
“Serikali kupitia TCRA imeendelea kutoa elimu na imekuwa na Programu Maalum za kuwaelimisha watumiaji wa mitandao kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao na kuendelea kufuatilia wanaokiuka maadili ya Mtanzania na kuwawajibisha ikiwemo kuwafungia uzalishaji wa maudhui na kuwapiga faini kwa mujibu wa Sheria za vyombo vya habari na za nje” – Mhe. Hamis Mwinjuma
“Serikali imeanzisha bodi ya Ithibati ya Waandishi wa habari ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016. Bodi hii inasimamia weledi na maadili kwa Waandishi na kuhakikisha Waandishi wenye sifa tu ndiyo wanaruhusiwa kutumika katika vyombo vya habari” – Mje. Hamis Mwinjuma
Akiuliza swali la nyongeza bungeni, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Tanzania, Mhe. Amina Ali mzee ameuliza; kumekuwa na ongezeko kubwa la vyombo vya habari vya mtandaoni, Je, bodi ya Ithibati inasimamiaje kuhakiki Waandishi wa habari?
“Bodi ya Ithibati lengo lake la msingi ni kuhakikisha inasimamia weledi na maadili miongoni mwa Waandishi wa habari wakiwemo Waandishi wa habari wa vyombo vinavyotekeleza majukumu yake mtandaoni ili kuhakikisha Waandishi wa habari wanafanya kazi kwa kufuat
a weledi, maadili na kuzingatia usalama wa Taifa bila kukandamiza Uhuru wa habari” – Mhe. Hamis Mwinjuma