Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitembelea Makumbusho ya Rais wa kwanza na Muasisi wa Taifa la Angola, Hayati António Agostinho Neto katika eneo la Public Square Jijini Luanda, tarehe 08 Aprili, 2025.
Rais Dkt. Samia amepokelewa kwa heshima ya kijeshi katika eneo hilo la Makumbusho na kisha kuweka shada la maua katika Mnara wa Kumbukumbu wa Rais wa kwanza na Muasisi wa Taifa hilo Hayati António Agostinho Neto.