Na Sabiha Khamis Maelezo
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh amesema ni muhimu kuyaenzi na kuyalinda Mapinduzi ya 1964 yaliyoasisiwa na viongozi kwa kufanya kazi kubwa ya kupigania uhuru wa nchi ili kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo.
Ameyasema hayo katika ziara ya kusoma dua katika kaburi la aliekua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mstaafu Marehemu Khamis Dawresh Mdigo na Kanali Mstaafu Marehemu Seif Bakari Omar, Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi B Unguja amesema viongozi hawa ni miongoni mwa viongozi wa kamati ya watu 14 walioleta Mapinduzi dhidi ya ustawi wa Wazanzibari.
Amesema viongozi hao wamejitolea maisha yao kwa kupigania uhuru wa nchi na kutaka ukombozi wa Wazanzibari na kuwewekea mazingira huru ya kujiletea maendeleo kwa vizazi vijavyo.
“Hivi sasa tunafurahia maisha tuliyotafutiwa na kutuanzishia na wazee wetu ambao ndio waasisi wa Mapinduzi ambao wamaifanya kazi kubwa ya kujitoleea kwao kufa ili tuwe na uhuru” alisema Naibu Waziri.
Amefahamisha kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kuilinda historia ya nchi na kutunza kumbukumbu ili kuweza kudumu na kutambuliwa na vizazi vijavyo.
Nae msoma risala Ndugu Bakari Omar Seif ameipongeza Serikali kwa jitihada wanazozichukua za kuwakumbuka viongozi na waasisi hao kwa kuwaombea hivyo wameomba kulidumisha na kuendeleza jambo hilo kwa vizazi vijavyo pamoja na kuiomba Serikali kuwatekelezea ibada ya Hijja viongozi hao ikawe saddaka itakayowafaa mbele ya Allah.
Kwa upande wake mwanafamilia Mwanakhamis Mohamed Mataka amewaomba vijana na jamii kwa ujumla wakumbuke jitihada za wazee waliopindua nchi kwa ajili ya kujiweka huru na kuleta amani na utulivu katika nchin ili kuendelea kuishi kwa salama, amani na uhuru katika kujiletea maendeleo.
Ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kusoma dua katika makaburi ya viongozi, waasisi wa Mapiduzi ya Zanzibar na Katibu wa kwanza wa Chama cha Afro Shirazi ambapo kilele kitafanyika Aprili 7, 2025 Kisiwandui Wilaya ya Mjini, Unguja.