Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati Mkutano wa Mawaziri kutoka Nchi zaidi ya 23 uliolenga kuweka mikakati ya ujumuishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mikakati na sera za nchi ili kuendelea kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu, mkutano umefanyika Mjini Berlin Nchini Ujerumani tarehe 01 Aprili, 2025.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Ngazi ya Mawaziri kutoka Nchi zaidi ya 23 uliolenga kuweka mikakati ya ujumuishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mikakati na sera za nchi wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Mjini Berlin Nchini Ujerumani tarehe 01 Aprili, 2025.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Dunia wa Watu wenye Ulemavu (Global Disability Fund – GDF) Dkt. Ola Abualghaib, akizungumza jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati Mkutano wa Mawaziri kutoka Nchi zaidi ya 23 uliolenga kuweka mikakati ya ujumuishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mikakati na sera za nchi ili kuendelea kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu, mkutano umefanyika Mjini Berlin Nchini Ujerumani tarehe 01 Aprili, 2025.
NA. MWANDISHI WETU , BERLIN UJERUMANI
Mfuko wa Dunia wa Watu wenye Wlemavu (Global Disability Fund – GDF) umezikutanisha nchi zaidi ya 23 Mjini Berlin Nchini Ujerumani huku wakijikita katika kuzungumzia masuala yanayohusu Watu Wenye Ulemavu katika nyaja mbalimbali ikiwemo Elimu, Mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi, kukabiliana na kurejesha hali wakati wa maafa pamoja na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Katika Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri kutoka Nchi zaidi ya 23 na kuweka mikakati ya ujumuishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mikakati na sera za nchi ili kuendelea kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu na kuwa na mazingira rafiki yenye kuwawezesha na kushiriki katika fursa mbalimbali.
Tanzania imeshiriki mkutano huo huku ikieleza namna Nchi ilivyojipanga kuhakikisha masuala ya Watu Wenye ulemavu yanapewa kipaumbele kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayosaidia katika utekelezaji ya masuala yanayowakabili watu wenye ulemavu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy Nderiananga ameeleza namna Tanzania inavyozingatia ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali ikiwemo Elimu, masuala ya mabadiliko ya Tabianch, fursa za uongozi, fursa za kiuchumi pamoja na masuala ya kijinsia.
Aidha amefafanua kuwa, Serikali itaendelea kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu hususani katika athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo uwepo wa maafa yanayoleta madhara mbalimbali ikiwemo vifo, uharibifu wa miundombinu pamoja na athari za kiuchumi.
Alieleza kuwa katika kutambua athari zitokanazo na maafa hususani kwa watu wenye ulemavu, Serikali itaendelea kuweka uangalizi mahususi katika shughuli za usimamizi wa maafa kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo huku wakitambua athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia Nchi Dunia.
“Sheria ya Usimamizi wa Maafa Sura 242 imeweka uwakilishi wa watu wenye ulemavu kwa Jukwa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa. Vilevile, Kanuni za Usimamizi wa Maafa za mwaka 2022 zinaelekeza kuzingatia mahitaji yao wakati wa kufanya tathmini ya madhara na mahitaji kwa ajili ya kukabiliana na maafa na kurejesha hali,”alisema
Aliongezea kuwa, Sheria ya Usimamizi wa Maafa Sura 242 imeweka uwakilishi wa watu wenye ulemavu kwa Jukwa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa. Vilevile, Kanuni za Usimamizi wa Maafa za mwaka 2022 zinaelekeza kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu wakati wa kufanya tathmini ya madhara na mahitaji kwa ajili ya kukabiliana na maafa na kurejesha hali.
Aidha,Tanzania inazingatia Mwongozo wa Kutoa Misaada ya Kibinadamu kwa Watu Walioathirika na Maafa wa mwaka 2022 unaelekeza kuweka kipaumbele kwa watu wenye ulemavu yaliyo katika kaya zisizo na uwezo au msaada wa ndugu na jamaa. Halikadhalika, miongoni mwa malengo ya Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa 2022 -2027 ni kuimarisha mchangamano wa jinsia, vijana, watu wenye ulemavu katika usimamizi wa maafa.
Naye Mkurugenzi wa Mfuko wa Dunia wa Watu wenye Ulemavu (Global Disability Fund – GDF) Dkt. Ola Abualghaib akifungua mkutano huo amesema ni wakati sahihi kwa watu wenye ulemavu duniani kuendelea kupaza sauti na kushirikiana katika masuala mbalimbali yenye kuleta chachu katika nyakati za ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu kwa kuzingatia namna dunia ilivyopiga hatua katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya kiteknolojia.
“Ni furaha leo tumekutana hapa Ujerumani katika kuelekea Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Masuala ya Watu wenye Ulemavu Duniani, ni vyema tukaendelea kuwa na juhudi za pamoja kuhakikisha kunakuwa na utekelezaji wa mipango inayotuhusu bila kumuacha yoyote nyuma,” alisema Dkt. Ola
Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Watu wenye Ulemavu Ujerumani, 2025 (Third Global Disability Summit) unafanyika Mjini Berlin, nchini Ujerumani kuanzia tarehe 02 hadi 03 aprili, 2025.Mkutano huo unalenga kujadili namna ya kuweka mikakati ya Ujumuishwaji wa masuala ya Watu wenye ulemavu katika nyanja mbalimbali.