MoonAliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, ameonesha kutoridhishwa na namna chama hicho kilivyoshughulikia taarifa za shambulio dhidi ya kiongozi wa wanawake wa chama hicho (BAWACHA). Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Mrema ametoa maoni yake kuhusu jinsi tukio hilo lilivyoripotiwa na chama, akionesha hisia za kusikitishwa na msimamo uliochukuliwa.
Mrema amehoji kwa nini chama hakikutoa tamko la wazi la kulaani shambulio hilo, badala yake kikiita taarifa hizo kuwa ni uvumi wa mitandaoni. Ameeleza kuwa hatua hiyo inaonesha udhaifu katika mshikamano wa chama na kutofanya juhudi za kumsaidia mhanga wa tukio hilo.
Pia, Mrema ameeleza kushangazwa na chama kushindwa kutoa pole kwa kiongozi huyo, akibainisha kuwa CHADEMA mara nyingi imekuwa ikitoa pole kwa watu wa makundi mbalimbali, hata kwa viongozi wa CCM wanapopatwa na matatizo.
Ameeleza kuwa kauli za chama kuhusu uchunguzi wa tukio hilo zimeambatana na vitisho kwa mhanga wa shambulio, jambo ambalo linatia wasiwasi juu ya dhamira halisi ya kufanikisha uchunguzi huo kwa haki.
Mrema pia ametoa changamoto kwa CHADEMA kujitathmini kuhusu namna inavyoshughulikia masuala ya haki za binadamu na haki za wanawake ndani ya chama. Amesema kuwa hali hii inafanana na kauli zilizowahi kutolewa wakati wa utawala wa Hayati John Magufuli, ambapo matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yalipingwa vikali na chama hicho.
Katika tamko lake, Mrema amesisitiza kuwa analaani vikali kitendo cha kiongozi wa wanawake