Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Arusha leo Machi 28, 2025 imekabidhi kompyuta kwa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa ajili ya matumizi ya mifumo ambayo inatummiwa kwa sasa na kikosi hicho katika kutoa huduma.
Vifaa hivyo vine kabidhiwa na Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Veronica Ignatus na kupokelewa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Kamati hiyo SSP. Zauda Mohamed pamoja na Maafisa, Wakaguzi na Askari kutoka kikosini hapo.
Aidha SSP Zauda amebainisha kuwa vifaa hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko ya kiutendaji ndani ya kikosi hicho ambacho kimejikita zaidi katika matumizi ya mifumo katika utoaji huduma.