Meneja miradi wa YEFFA ,AGRA ,Donald Mizambwa akizungumza na waandishi wa habari katika mjadala huo jijini Arusha leo.

Afisa biashara mkoa wa Arusha, Njivaine Mollel akizungumza na waandishi wa habari katika mjadala huo mkoani Arusha leo.

Mkurugenzi wa TCCIA ,Oscar Kissanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

………….
Happy Lazaro, Arusha .
Zaidi ya vijana 110 kutoka maeneo mbalimbali mkoani Arusha wamekutana mkoani Arusha katika mjadala wa kuongeza ushiriki wa wafanyabiashara wa mazao ya kilimo wanaoongozwa na wanawake na vijana ,pamoja na kuongeza kiasi cha biashara ya mipakani katika minyororo muhimu ya thamani ya bidhaa zitokanazo na kilimo .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha katika ufunguzi wa mjadala huo, Meneja miradi wa YEFFA ,AGRA ,Donald Mizambwa amesema kuwa ,lengo ni kuona vijana hawa wanapata fursa zilizopo katika sekta ya Kilimo .
Amefafanua kuwa,Programu hiyo ilianza julai , 2024 katika kipindi hicho hadi sasa wameshafikia vijana 140,000 ambao wamepata zile fursa zilizopo kwenye kazi na bado kazi inaendelea huku lengo likiwa ni kufikia vijana 261,000 ambao wamepata fursa za kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu .
Amesema kuwa ,Shirika la AGRA ni shirika lisilo la kiserikali ambalo linashirikiana na serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo katika kuhakilisha kuwa wanaleta maendeleo kwenye sekta ya kilimo .
Amesema kuwa, kuanzia mwaka 2020/24 AGRA kwa kushirikiana na serikali wanatekeleza mradi unaojulikana kwa jina la EFFA mradi unaofadhiliwa na Mastercard Foundation kwa kushirikiana na AGRA pamoja na wadau wengine wa maendeleo .
Amesema kuwa, mradi huo unafanyika katika mikoa 18 Tanzania Bara pamoja na.Visiwani .
“taribani wiki tatu sasa hadi wiki nne walikuwa wanafanya midahalo pamoja na wadau wa serikali na vijana katika kuangalia ushiriki wa vijana katika sekta ya kilimo kwani mradi huo lengo lake ni kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo kwani kwenye kilimo kuna fursa mbalimbali ikiwemo biashara za mipakani hivyo kwenye mdahalo huo kuna wale vijana wanafanya biashara za mipakani lakini wengine hawafanyi ila wanatamani kufanya hizo biashara “amesema .
Amesema kuwa,kupitia wadau mbalimbali wa serikali ambao wapo kwenye sekta muhimu wanakuja kutoa mawasilisho mbalimbali kuhakikisha vijana hawa wanaelimika na kujua fursa zilizopo .
Ameongeza kuwa, walianzia mkoa wa Mbeya ,Songwe Kigoma,Kagera ,na Mwanza , Mara na kuja Arusha leo huku lengo ni kuona vijana hawa wanapata fursa zilizopo katika sekta ya Kilimo .
“Tunaposema vijana tunamaanisha wale wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 35 na kati ya hao lengo la mradi ni kuhakikisha asilimia 80 ya vijana wananufaika na asilimia hiyo 80 ni vijana wa kike “amesema .
Amesema wanalenga vijana wa kike kwani wengi wanasahaulika na kuonekana ni wa kukaa nyumbani wakati sivyo bali wana fursa na nafasi kubwa ya kuingia katika sekta ya uzalishaji kwani mipakani kuna fursa nyingi sana kwa vijana lengo katika mdahalo huu vijana wazitambue hizo fursa zilizopo ndani na nje ya Tanzania katika mazao ya chakula .
Kwa upande wake Afisa biashara mkoa wa Arusha, Njivaine Mollel akizungumza katika mafunzo na majadiliano hayo amesema kuwa,mradi huo unafadhiliwa na AGRA kupitia program ya Ujasiriamali wa vijana kwa mustakabali wa chakula na kilimo (YEFFA) na kutekelezwa na TCCIA ambapo kwa pamoja wameamua kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara katika mipaka ya mikoa ya Mbeya,Songwe,Kigoma,Kagera, Shinyanga,Mara na Arusha kwa kupunguza vikwazo visivyo vya kiforodha ,kutumia utaratibu uliorahisishwa kwa wafanyabiashara wadogobna wa kati.
Pamoja na kuwafundisha namna ya kutumia mitandao kuboresha masoko ya bidhaa wanzouza nchi za jirani na hata nchi za kimataifa, na kuwafundisha njia za kupata mikopo ili kuinua mitaji ya biashara wanazofanya.
“Mradi huu unalenga kupunguza vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiforodha kutumia utaratibu uliorahisishwa kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati na kuboresha mazingira ya biashara ya bidhaa za kilimo kwa wafanyabiashara wadogo hasa vijana na akinamama katika mipaka ya nchi yetu.”amesema .
Naye Mkurugenzi wa TCCIA ,Oscar Kissanga amesema kuwa,mjadala huo unalenga kuongeza ushiriki wa wafanyabiashara wakina mama na vijana wa bidhaa za kilimo (mahindi ,mchele,maharage,soya,matunda na mbogamboga)ili kuongeza kiwango cha biashara ya mipakani katika bidhaa hizo .
Amesema kuwa, wanataka kuwezesha vijana na akina mama kushiriki katika soko la ndani na Afrika Mashariki na kuwezesha maisha yao katika kuhakikisha wanafanya biashara na kuchangia pato la Taifa na nchi kwa ujumla.