Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amewataka viongozi wa Dini kusaidia Serikali katika mapambano ya dhidi ya Vitendo vya Ukatili na Mmomonyoko wa maadili ulinzi na Aman kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Mtambi ametoa kauli hiyo Wakati alipowaalika viongozi wa Dini katika Futari Ikulu ndogo ya Mkoa wa mara ambapo amewataka kuwa sehemu ya kukemea watu ama kundi linalojaribu kupotesha Dhidi ya utulivu uliopo nchini.
“Niwaombe Sana viongozi wa Dini tusaidieni katika hili kwenye maeneo yenu hasa ya ibaada tuanahitaji kila moja kuwa mlinzi wa Iman yetu nakuhakikisha hadi hapa alipotufikisha DKT Samia Suluhu Hassan tunapalinda.
Mtambi amewakumbusha viongozi wa Dini kukumbuka kukemea Mmomonyoko wa maadili kwenye jamii inayowazunguka Kufuatia kuwepo kwa viashiria vinavyoonesha maadili kuharibika miongoni mwa vijana.
Katika hatua nyingine RC Mtambi amesema Serikali itashirikiana na viongozi hawa katika kuunganisha nguvu katika mapambano Dhidi ya Vitendo viovu.