Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe alipozindua Ujenzi wa Lango la Utalii Ndea lililopo kwenye Hifadhi ya Taifa Mkomazi wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro Machi 25, 2025. Wengine kutoka kushoto ni Kamishina Mkuu wa TANAPA , Juma Kuji, Katibu wa CCM Mkoa Kilimanjaro, Mercy Mollel, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu na kulia ni Mbunge wa Mwanga Wakili Thadayo Anania . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Ujenzi wa Lango la Utalii Ndea lililopo katika Hifadhi ya Taifa Mkomazi wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro Machi 25, 2025. Wengine kutoka kushoto ni Kamishina Mkuu wa TANAPA , Juma Kuji, Katibu wa CCM Mkoa Kilimanjaro, Mercy Mollel, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, Mbunge wa Mwanga Joseph Tadayo na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mwanga, Mwanahamisi Munkunda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wananchi wakati alipozindua Ujenzi wa Lango la Utalii Ndea kwenye Hifadhi ya Taifa Mkoamazi wilayani Mwanga, Machi 25, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza wakati alipozindua Ujenzi wa Lango la Utalii Ndea katika Hifadhi ya Taifa Mkoamazi wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro Machi 25, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkoamazi , Emmanuel Mwailama alipozindua Ujenzi wa Lango la Utalii Ndea katika Hifadhi ya Taifa Mkomazi Mkoani Kilimajaro, Machi 25, 2025. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
…………….
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuanzisha programu za kutangaza vivutio vilivyopo katika Tifadhi ya Taifa ya Mkomazi ili kuongeza idadi ya watalii wanaoingia katika hifadhi hiyo.
Amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa ikiwemo ujenzi wa barabara, lango la watalii na huduma nyingine za kijamii ndani ya hifadhi hiyo hivyo ni lazima sasa Mamlaka hiyo itumie fursa hiyo kuongeza idadi ya watalii.
Ametoa maagizo hayo leo (Jumanne Machi 25, 2025) alipokuwa akizungumza na wahifadhi na wananchi baada ya kuzindua lango la kuingia na kutoka watalii la Ndea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lililoko Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
“Tutangaze mbuga yetu ya Mkomazi na vivutio vyake, wanyama ambao hawapatikani maeneo mengine watamkwe sana kwamba wanapatikana hapa, elezeeni umbali wa kutoka Moshi na Tanga mjini hadi hapa hifadhini.”
Amesema ujenzi wa lango hilo ni sehemu ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuchochea na kuongeza vivutio vya utalii nchini.
Aidha, ameiagiza TANAPA kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa zinazopatikana kutokana na uwepo wa watalii ikiwemo vitu vinavyopendwa na watalii ili waweze kunufaika huku akiwataka wanananchi kuchangamkia fursa hizo.
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa kuweka mkakati wa kuimarisha mawasiliano katika njia na maeneo yaliyoko ndani ya hifadhi hiyo.
“Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nayo ihakikishe kunakuwa na mawasiliano ya uhakika katika maeneo ya mbuga hiyo.”
Akitoa taarifa juu ya manufaa ya lango hilo Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Emmanuel Mwailama amesema ujenzi wa lango hilo utaongeza idadi ya watalii katika mbuga hiyo ambao wengi wanakwenda kuona maisha ya jamii ya ziwa jipe, Faru weusi pamoja na Tembo.
Amesema pia lango hilo litachochoe fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo la hifadhi kutokana ongezeko la watalii watakaopita njia hiyo ikiwa ni pamoja na kutengeneza ajira kwa wakazi wa vijiji vya eneo hilo.
Ujenzi wa lango hilo limegharimu Shilingi Milioni 350 na lina ofisi za idara nyingine za serikali kama Uhamiaji, Mamlaka ya mapato na benki.