UONGOZI WA AWAMU YA SITA KATIKA KASI YA MAENDELEO
Katika miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania imepiga hatua kubwa katika uchumi, jamii, na diplomasia. Kwa uongozi wake thabiti, ameimarisha demokrasia, ameboresha miundombinu, elimu na afya, pamoja na kukuza usawa wa kijinsia kwa wanawake na vijana. Juhudi zake za kuimarisha ushirikiano wa kimataifa zimeleta fursa mpya za uwekezaji na maendeleo. Jiunge nasi kutathmini mafanikio, na mustakabali wa taifa letu.
SEKTA YA UCHUKUZI
Kwenye sekta ya uchukuzi, serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 01 Agosti, 2024,ilizindua rasmi safari za treni ya SGR kutoka Dar es salaam mpaka Dodoma. Mradi huu wa kimkakati uliendeleza kilometa 722 zilizokuwa zinajengwa mwaka 2021 hadi kufikia kilometa 2,102 zilizojengwa mwishoni mwa mwaka 2024.
Tangu kuanza kwa safari za treni ya SGR, Serikali kupitia TRC imesafirisha zaidi ya abiria milioni mbili (2,000,000 ) na kuwezesha kukusanya maduhuri yenye jumla ya Shilingi bilioni 54 mpaka kufikia mwezi machi 2025 .
Rais Samia Suluhu Hassan, amefanikisha upatikanaji wa fedha za ujenzi wa reli ya SGR kutoka Tabora – Kigoma Km 506 ambayo itafungua mipaka ya biashara na nchi ya Demokrasia ya Kongo kupitia ziwa Tanganyika (Kigoma).
Katika kuimarisha usafiri wa anga nchini, tangu Mhe. Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, zimenunuliwa ndege saba na kuifanya ATCL kuwa na ndege 14 mpya za kisasa za abiria na ndege moja ya mizigo zinazohudumia vituo vya ndani, kikanda na kimataifa.
Uwekezaji huu umeiwezesha ATCL kuongeza idadi ya abiria na mapato. Idadi ya abiria wa ATCL imeongezeka kutoka Abiria 822,232 mwaka 2021/22 hadi abiria 1,123,696 mwaka 2023/24. Kwa upande wa mapato, ATCL imefanikiwa kuongeza mapato kutoka shilingi 254 bilioni mwaka 2021/22 hadi shilingi 464.5 bilioni mwaka 2023/24.
Pamoja na hayo yote, Serikali ya Tanzania imejikita katika kutanua na kuboresha bandari za Dar es Salaam, Tanga, na Mtwara.Pamoja na kuzindua bandari mpya ya Mbamba bay,
Serikali kupitia TPA inaendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa
uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, wenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 421.
Mradi huu unatarajiwa kuongeza uwezo wa bandari kutoa huduma kwa meli kubwa za kisasa na kuboresha ushindani wa bandari ya Dar es Salaam katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
SEKTA YA NISHATI
Sekta ya nishati nchini imepitia mabadiliko makubwa. Kufikia Februari 2025, uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini umeongezeka hadi megawati 3,796.71, zaidi ya mara mbili ya megawati 1,889.84 zilizorekodiwa Januari 2024.
Maendeleo haya makubwa ni ushahidi wa juhudi za taifa kuwasha mustakabali wa serikali ya awamu ya sita ya kukuza uchumi endelevu kupitia matumizi ya nishati safi na ya kisasa, huku ikichochea maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 umefikia asilimia 99.8. Kwa sasa, mashine 8 kati ya 9 zimeanza kuzalisha jumla ya megawati 1,880, huku mashine moja iliyobaki ikitarajiwa kukamilika Februari 2025. Mradi huu umeondoa mgao wa umeme, kuzima mitambo ya gharama kubwa ya mafuta, na kuimarisha upatikanaji wa umeme vijijini, kwenye treni ya SGR, na maeneo yasiyokuwa na umeme.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kinara wa ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia nchini na Barani Afrika, pamoja na kuzindua mkakati wa taifa wa Nishati Safi, anaendelea kuinadi ajenda hiyo katika jukwaa la kimataifa. Lengo lake ni kuhakikisha kuwa watu wanapika katika mazingira salama kiafya na kimazingira.
Vilevile Rais Samia aliweka historia nchini alipoongoza Mkutano wa Nishati barani Afrika uliiohudhuriwa na Wakuu wa nchi 22. Malengo ya Mkutano yalikuwa kuweka mkakati mahususi ya kahikisha watu 300 barani Afrika kupata umeme ifikapo mwaka 2030. Mataifa 12 ya Afrika, ikiwemo Tanzania, yalizindua Mipango ya Kitaifa ya Nishati (National Energy Compact 2025-2030).
SEKTA YA AFYA
Wahenga wanasema ‘Afya ni mtaji.’Chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, sekta ya afya ya Tanzania imepata mafanikio makubwa katika miaka minne iliyopita.
Serikali pia imeongeza vifaa vya kisasa vya matibabu, ikiwa ni pamoja na mashine 13 za MRI, 45 za CT Scan, 491 za Digital X-Ray, na 970 za Ultra Sound, ambazo sasa zinapatikana hadi kwenye zahanati.
Uwezo wa wataalam wa afya umeimarishwa, na kupitia mpango wa Samia Health Specialization Scholarship, madaktari bingwa 1,455 walipata mafunzo, na idadi ya madaktari bingwa ikaongezeka kutoka 2,637 hadi 2,684 mwaka 2024.
Huduma za uzazi na dharura zimeimarishwa, na vituo vinavyotoa upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni vimeongezeka kutoka 388 hadi 523. Mfumo wa M-Mama, unaotoa usafiri wa haraka kwa wajawazito, umewafikia zaidi ya 105,780 wanawake nchini.
Uongozi wa Rais Samia umetambuliwa kimataifa, ambapo ameteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa Championi wa Dunia wa Usawa wa Kijinsia, na amepokea Tuzo ya The Global Goalkeepers kutoka Gates Foundation kwa mafanikio makubwa katika sekta ya afya ikiwemo kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 80.
SEKTA YA MAJI
Msemo maarufu usemao “Maji ni uhai” umepewa kipaumbele kikubwa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Upatikanaji wa maji vijijini umeongezeka kutoka asilimia 70.1 hadi 79.6, huku mijini ukiwa umeongezeka kutoka asilimia 84 hadi 90. Miradi 1,633 ya usambazaji wa maji imekamilika, ikiwa ni pamoja na miradi 1,335 vijijini na 298 mijini.
Katika kulinda vyanzo vya maji, serikali imezindua Kampeni ya Kitaifa ya Upandaji Miti Rafiki wa Maji. Ambapo tayari miti milioni 2,541,803 imepandwa katika mabonde yote tisa nchini.
Kwa hatua hizi zote na nyingine nyingi, Tanzania inasonga mbele kuelekea upatikanaji endelevu wa maji safi na salama kwa maendeleo ya taifa.
UWEKEZAJI
Kuanzia kuimarisha ushiriki wa serikali hadi kuvutia uwekezaji wa kimataifa, mafanikio ya sekta ya uwekezaji yamekuwa ya kuvutia.
Serikali imeongeza umiliki wake wa hisa katika Kampuni ya Madini ya Almasi ya Williamson kutoka asilimia 25 hadi 37. Pia, kupitia mikataba ya ubia, serikali imeweza kumiliki hisa zisizohamishika katika kampuni saba za madini na uchimbaji, ikiwemo Faru Graphite, Kudu Graphite, na Tembo Nickel Refining Limited.”
Kupitia Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji ya Mauzo ya Nje (EPZA), uwekezaji wa zaidi ya dola bilioni 1.17 umevutiwa nchini. Miradi 45 iliyosajiliwa imeleta ajira zaidi ya 20,000 na kuongeza mauzo ya nje kwa thamani ya dola milioni 397.64.”
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi 901 mwaka 2024, ikivunja rekodi ya miradi 885 iliyosajiliwa mwaka 2013. Miradi hii imeimarisha sekta za kilimo, viwanda, na bidhaa za madini.”
Kwa kuunganisha taasisi kama TIC na EPZA, serikali imeondoa mwingiliano wa majukumu na kuweka mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji zaidi.”
SEKTA YA MADINI
Serikali imeweka msisitizo kwenye uongezaji thamani wa madini ili kuhakikisha inapata faida kwa taifa na wananchi.
Kupitia ushirikiano wa kimataifa na uwekezaji wa kimkakati, Tanzania inajitokeza kuwa kitovu cha madini Afrika Mashariki na duniani.
Maboresho na usimamizi wa Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko ya madini na vituo vidogo vya ununuzi wa madini, makusanyo ya maduhuli ya Serikali yameongezeka kutoka shilingi bilioni 161 mwaka 2015/16 hadi kufikia shilingi bilioni 756 mwaka 2023/24.
Aidha, kuanzia kipindi cha Julai hadi Desemba 31, 2024 kiasi cha kilikuwa kimekusanywa sawa na asilimia 52.15 kwa lengo la mwaka 2024/25 ya kukusanya shilingi trilioni 1.
Serikali imeendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha wachimbaji wadogo na kuhakikisha wanaendelezwa kwa kusogezewa huduma za ugani pamoja na kuwekewa mazingira mazuri ili wafanye shughuli zao kwa tija.
TAMISEMI
Serikali kupitia TAMISEMI imefanya kazi ya kutambua na kukusanya takwimu za masoko 1,415 katika halmashauri 184 ilipofika Desemba 2024..
Mpaka sasa Serikali imesajili vikundi 4,073 vya huduma ndogo za fedha, kufikia jumla ya vikundi 56,645 vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu nchini. Pia, imeanzisha mfumo mpya wa utoaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2024/25. Hadi Desemba 2024, vikundi 2,726 vimepata mikopo ya shilingi bilioni 27.67 kutoka halmashauri 64, huku shilingi bilioni 27.76 zikitokana na mapato ya halmashauri na milioni 93.1 kutoka marejesho ya mikopo.
Serikali inaendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga shule mpya 234 za kata, shule 103 za sekondari za amali, na shule saba za bweni za wavulana pamoja na nyumba za walimu 229.
Zaidi ya shilingi bilioni 9.35 zimetumika kununua vifaa vya TEHAMA kwa shule 231 za sekondari, zikiwemo kompyuta, projectors, na vifaa vingine vya kidigitali.
SEKTA YA ARDHI
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imepata mafanikio makubwa katika usajili na ugawaji wa ardhi. Hadi sasa, Hati Miliki zaidi ya laki moja 101,474 zimetolewa kwa wananchi. Pia, sehemu za majengo 252 imesajiliwa, na nyaraka za kisheria 123,583 zimeshaandaliwa. Hati za Hakimiliki za Kimila 5,042 zimetolewa kwa wananchi katika halmashauri mbalimbali nchini.”
Wizara pia imepitisha Sera ya Ardhi ya mwaka 2023 na inaendelea kuboresha Sera ya Maendeleo ya Makazi ili kuhakikisha usimamizi bora wa sekta ya nyumba na kuongeza tija. Mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya yameongezeka kutoka 59 hadi 115, na zaidi ya kesi 110,000 zimepata maamuzi.
Jitihada za kurasimisha makazi yasiyo rasmi zinaendelea, ambapo jumla ya nyumba 143,810 zimepata umaarufu katika halmashauri mbalimbali.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linaendelea na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Huku Nyumba 1,015 zimekamilika, 387 zikiwa zimekamilika kabisa na nyumba 628 ziko kwenye hatua ya ukamilishaji.
SEKTA YA KILIMO
Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania. Chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, sekta ya kilimo imepiga hatua kubwa katika miaka minne iliyopita. Bajeti ya kilimo imeongezeka kwa asilimia 230, kutoka Shilingi Bilioni 294 mwaka 2021/2022 hadi Shilingi Bilioni 1,248 mwaka 2024/2025.”
Kwa kuanzisha Benki ya Taifa ya Ushirika kwa mtaji wa Shilingi Bilioni 20, wakulima sasa wanapata mikopo yenye riba ya chini kama asilimia 4.5. Serikali pia imeshawishi taasisi za fedha kupunguza riba kutoka 22% hadi 9%, jambo linalochochea uwekezaji zaidi katika kilimo.
Kupitia Kituo cha Huduma za Ushauri kwa Wakulima (M-Kilimo), utoaji wa huduma za ugani umeimarishwa. Pia, sekta ya kilimo imefungamanishwa na viwanda, ikiongeza thamani ya mazao yetu
Vilevile, Mauzo ya mazao ya kilimo nje ya nchi yameongezeka maradufu, kufikia dola bilioni 2.3, na kuimarisha nafasi ya Tanzania kwenye soko la dunia.”
Huku, Kilimo cha mazao ya biashara kikipiga hatua pia. Uzalishaji wa alizeti pekee umeongezeka kwa asilimia 136.4, huku mazao kama tumbaku, pamba, na korosho yakivutia wawekeza ji.
Kupitia programu ya ‘Jenga Kesho Iliyo Bora,’ vijana 686 wamepewa mashamba kwa ajili ya kilimo biashara, wakijenga mustakabali mzuri wa maisha yao.
Teknolojia pia inachangia kukabiliana na changamoto. Serikali imenunua ndege nyuki 41 kwa ajili ya kudhibiti wadudu waharibifu na kulinda mavuno ya wakulima.
SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI
Serikali imeanzisha masoko tisa ya mifugo, huku manane yakiwa hatua za mwisho kukamilika. Vituo vitano vya ukusanyaji wa maziwa vimejengwa na vingine vitano vinaendelea kujengwa.
Sekta ya uvuvi ikichangia 1.7% kwenye Pato la Taifa na kutoa ajira kwa zaidi ya watu milioni sita. Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko umekamilika kwa 79% na unatarajiwa kuajiri watu 570.
Mauzo ya samaki nje ya nchi yaliongezeka kutoka tani 42,371.41 zenye thamani ya TSh 509.9 bilioni ($213.4 milioni) mwaka 2023 hadi tani 59,746.41 zenye thamani ya TSh 775.9 bilioni ($289.6 milioni) mwaka 2024.
Huku hatua za serikali dhidi ya uvuvi haramu zimechangia kupunguza uvuvi wa baruti katika pwani.
MALI ASILI NA UTALII
Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kutangaza utalii wa Tanzania kupitia filamu za kimkakati, zikiwemo The Royal Tour na Amazing Tanzania. Filamu hizi zimeongeza idadi ya watalii kutoka 1.8M mwaka 2023 hadi 5.4M mwaka 2024, na mapato ya utalii yakiongezeka kutoka USD milioni 3.3 hadi USD milioni 3.9.
Vilevile, Tanzania imetambulika zaidi kimataifa na kuweza kupata tuzo za World Travel Awards (WTA) pamoja na Africa’s Leading Destination (2024), World’s Leading Safari Destination (2024), na Hifadhi ya Taifa Serengeti kuendelea kuwa bora Duniani kwa miaka sita mfululizo. Mlima Kilimanjaro pia umejizolea sifa kubwa kwa kushinda African Leading Tourism Attraction (2024), huku Bodi ya Utalii ikishinda Africa’s Leading Tourism Board. Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Tuzo za World Travel Awards kwa Ukanda wa Afrika na Bahari ya Hindi mwaka 2025.
Katika muendelezo wa kutangaza utalii kwenye nchi ambazo ni masoko ya kimkakati, wizara iliratibu Roadshow katika Miji ya Shanghai na Guangzhou nchini China ambapo iliambatana na kampuni za utalii zaidi ya 30 kutoka nchini. Aidha, kampuni hizo zilipata fursa ya kukutana na makampuni ya utalii takribani 400 ya nchini China na kuanzisha mashirikiano ya kibiashara katika kuvutia watalii kutembelea Tanzania
Tanzania imefanikiwa kuwa mwenyeji wa matukio mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo Jukwaa la Pili la Utalii wa Chakula Duniani kwa Kanda ya Afrika linaloandaliwa na Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) lililopangwa kufanyika mwezi Machi, 2025 Jijini Arusha. Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika Mwezi Januari, 2025 Jijini Dar es Salaam ambapo uliitangaza nchi yetu kimataifa kama Kituo Bora cha Utalii (Award Winning Destination); Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CHAN) yaliyopangwa kufanyika Agosti, 2025 ambapo ni fursa adhimu ya kutangaza vivutio vyetu vya utalii ikizingatiwa kuwa michezo huusisha mashabiki wengi kutoka mataifa mbalimbali ya kikanda barani Afrika; Mkutano wa 73 wa Baraza la Viwanja vya Ndege Afrika uliopangwa kufanyika Aprili, 2025 Jijini Arusha.
WIZARA YA SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Chanda chema huvikwa pete! Historia imeandikwa katika sekta za utamaduni, sanaa na michezo katika kipindi kifupi cha miaka minne ya uongozi wake utamaduni wetu umepata nguvu mpya, matamasha na makongamano yameimarika, yakileta ajira, kukuza utalii wa kiutamaduni na mshikamano wa kitaifa
Kwa uamuzi mgumu wa Mheshimiwa Rais, Mfuko wa Utamaduni na Sanaa umefufuliwa tangu ulipokufa 2002, ukiwezesha wasanii kwa mikopo na kuwaunganisha na masoko ya kimataifa.
Aidha, Mfumo wa hakimiliki umeimarishwa, Wasanii sasa wanakusanya mirabaha yao wenyewe kupitia usimamizi wa COSOTA.”
Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake mwaka 1957, Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) yatafanyika Tanzania kwa ushirikiano na nchi za Kenya na Uganda. Pia imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya CHAN yatakayofanyika nchini Tanzania mwezi Agosti 2024.
Mashindano haya ya AFCON yatachagiza kuwapo kwa fursa lukuki za ujenzi wa miundombinu, kujenga uchumi, kuvutia utalii, ajira na kuitangaza Tanzania kimataifa.
Kwa mara ya kwanza, michezo kwa watu wenye ulemavu imepewa kipaumbele.Tembo Warriors wameipa Tanzania heshima kimataifa, huku Serengeti Girls wakifanya historia kwenye Kombe la Dunia.
Serikali imeanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Michezo kusaidia timu za Taifa kushiriki mashindano ya kimataifa, kukuza vipaji, kuboresha miundombinu, kulipa mshahara wa kocha wa Taifa Stars, na kuwajengea uwezo viongozi wa michezo. Kupitia mfuko huu, Shilingi bilioni 9.006 zimetolewa, zikichangia mafanikio makubwa katika sekta ya michezo nchini..
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Katika kipindi cha miaka minne, Wizara ya Mambo ya Ndani imepiga hatua kubwa katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao. (Je Start here)Jumla ya Polisi Kata/Shehia 4,349 wameajiriwa na shilingi bilioni 29 zimetumika kununua magari mapya ya polisi, pikipiki na boti za uokoaji ili kuongeza ufanisi wa majukumu ya usalama.
Aidha, sekta ya zimamoto na uokoaji imeboreshwa kwa kupata magari mapya ya kuzima moto, boti za uokoaji, huku mpango wa dola milioni 100 ukiandaliwa kwa ajili ya vifaa vya kisasa vya dharura, ikiwemo helikopta.
Huduma za uhamiaji zimeimarishwa kwa kutoa zaidi ya hati za kusafiria za kielektroniki 149,000, visa za mtandaoni 1.1 milioni, na vibali vya ukaazi 28,000, hivyo kurahisisha safari na uwekezaji nchini.
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imefanikiwa kusajili 79.5% ya watu wazima na kusambaza zaidi ya vitambulisho milioni 20 vya uraia, hatua inayochochea upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
WIZARA YA MAMBO YA NJE
Katika kipindi cha miaka minne, Tanzania kupata heshima na kutambulika katika majukwaa mbalimbali kikanda na kimataifa. Serikali ya awamu ya sita imeandaa na kushiriki mikutano mikubwa ya kimataifa ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kibiashara, hivyo kufungua fursa zaidi kwa maendeleo ya taifa.
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia alishiriki katika Mkutano wa katika Mkutano wa G20 uliofanyika Rio de Janeiro, Brazil. Kupitia mkutano huo, ambao Tanzania ilipata mwaliko wa kushiriki kutoka kwa Rais wa Brazil Mheshimiwa Lula De Silva kwenda kwa Rais wa Jamhurri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ushiriki wa Tanzania katika Mkutano huo umekuwa kielelezo cha heshima kubwa kwa nchi, na kutambulika kwa mchango wa Tanzania katika masuala ya kimataifa.
Miongoni mwa mikutano hiyo ni ; Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, Mkutano wa pamoja wa EAC na SADC kuhusu amani katika DRC, na Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC). Mikutano hii imeimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kibiashara, hivyo kufungua fursa zaidi kwa maendeleo ya taifa.
Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imefanikiwa kuimarisha ujirani mwema na nchi mbalimbali, jumuiya za kikanda na kudumisha amani na usalama katika kanda. Pia imeendelea kuchangia vikosi katika misheni za kulinda amani kikanda na kimataifa ambapo wanajeshi wake wamekuwa wakishiriki katika misheni za kikanda na kimataifa katika nchi za Msumbiji, DRC, Afrika ya Kati, Lebanon na nyinginezo
Katika masuala ya mazingira, Tanzania ilishiriki katika Mkutano wa COP29 nchini Azerbaijan, ikitoa msimamo wake kuhusu umuhimu wa hatua madhubuti za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa ujumla, mikutano na ziara hizo zina matokeo chanya kwa Taifa na zinachangia kuvutia wawekezaji kutoka nje ya nchi, kuongezeka kwa miradi ya maendeleo, kuongezeka kwa watalii na upatikanaji wa mikopo yenye masharti nafuu.
UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA
Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha dhamira ya kujenga utumishi wa umma wenye ufanisi kwa maendeleo ya taifa kupitia hatua mbalimbali za maboresho. Kwa mwaka 2024, serikali imewapandisha vyeo watumishi wa umma 234,121 kwa gharama ya shilingi bilioni 59.38, pamoja na kulipa malimbikizo ya mishahara ya watumishi 21,955 waliopo kazini yenye thamani ya shilingi bilioni 28.51.
Vilevile wastaafu 1,416 wamelipwa malimbikizo ya mishahara yenye jumla ya shilingi bilioni 5.42, huku watumishi 11,288 wakipandishwa madaraja mapya ya kazi na mishahara mipya kufikia shilingi bilioni 931.82.
Katika jitihada za kuimarisha rasilimali watu katika taasisi za umma, serikali imeajiri watumishi wapya 47,404 ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mbali na ajira na nyongeza za mishahara, Rais Samia amesisitiza nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma, jambo ambalo limeimarisha mifumo ya usimamizi wa rasilimali watu.
WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI
Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta ya mawasiliano kati ya 2020 na 2024. Mkongo wa Taifa umeongezeka kwa 66%, huku wilaya zilizounganishwa zikifikia 109 kati ya 139.
Matumizi ya simu yameongezeka kwa 69.46%, watumiaji wa intaneti kwa 45.41%, na gharama za intaneti na simu kushuka kwa kiasi kikubwa.
Miundombinu imeboreshwa kwa kuongeza minara, kusajili anwani milioni 12.8, na kuboresha mifumo ya TEHAMA. Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na mikakati ya uchumi wa kidijitali imeanzishwa, huku shule 30 zikifaidika na maabara za kompyuta na intaneti.
SEKTA YA KATIBA NA SHERIA
Na kwa upande wa wizara ya Katiba na Sheria imeweza kuhakikisha utawala wa sheria kwa kusimamia utoaji wa haki, hifadhi ya Katiba, na kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali. Pia, inahakikisha sheria zinakidhi mahitaji ya mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, na kiteknolojia.
Elimu ya uraia na utawala bora imetolewa kwa viongozi 1,401 katika mikoa mitano, na maudhui ya Katiba yameingizwa kwenye mitaala ya shule na vyuo vya ufundi stadi, ambapo VETA itaanza kufundisha mwaka 2024/2025. Serikali pia imeandaa muswada wa (Samia legal aid) marekebisho ya sheria za haki jinai.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imefikia wananchi 2,191,274 katika mikoa 22. Ili kuongeza ufanisi wa utoaji haki, mifumo mitatu ya TEHAMA imeunganishwa na Dashibodi ya Takwimu, ikihusisha Mahakama, RITA, na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Huduma za usajili wa vizazi, vifo, ndoa, na talaka zinapatikana kidijitali kupitia eRITA, huku mifumo ya GoTHoMIS na DHIS2 ikirahisisha usajili wa vizazi na vifo. Mifumo ya Marekebisho ya Sheria (LRMIS), Usajili wa Mashauri (CIMS), na OAG-MIS pia inaboreshwa kwa upatikanaji wa sheria, tafsiri, na mikataba mtandaoni.
Dawa za kulevya
Serikali ya awamu ya sita, imeweka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imepiga hatua kubwa katika kupunguza uingizaji, uzalishaji, na usambazaji wa dawa za kulevya nchini Tanzania.
Kwa kushirikiana na vyombo vya dola, zaidi ya kilogramu 2.3 milioni za dawa za kulevya zilinaswa mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la 18.53% ikilinganishwa na mwaka 2023.
Katika jitihada za kupunguza madhara ya dawa za kulevya, Mamlaka inaendelea kusimamia tiba ya Methadone katika vituo 16 vilivyosajiliwa waathirika 18,017, pamoja na kuratibu huduma katika nyumba 62 za upataji nafuu kwa waraibu 16,894.
Katika ngazi ya kikanda na kimataifa, Mamlaka iliimarisha ushirikiano kwa kusaini makubaliano na nchi za Zambia, Msumbiji, na Afrika Kusini, pamoja na mashirika kama UNODC na INCD.
ELIMU
Kuna usemi usemao ‘Mafanikio hayajifichi wala hayahitaji kuyatafuta kwa darubini.’ Usemi huu umepata tafsiri halisi tunapozungumzia mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta ya elimu nchini Tanzania.”
Tarehe 1 Februari, Mwaka 2025, Tanzania ilishuhudia mwanzo mpya wa elimu yetu, baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuzindua rasmi Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023.”
Sera hii inatoa mwelekeo mpya unaozingatia maarifa, stadi na ujuzi, ikilenga kuandaa rasilimali watu yenye ujuzi kama mtaji, ‘Human Capital.’ Pamoja na msisitizo mkubwa katika stadi za karne ya ishirini na moja, na mahitaji ya kiujuzi kitaifa, kikanda na kimataifa.”
Kwa kuhamasisha masomo ya Sayansi, serikali imeanzisha Samia Scholarship kwa wanafunzi waliovuma katika masomo ya sayansi, uhandisi, teknolojia na elimu tiba. Hadi kufikia mwaka 2023/24, zaidi ya wanafunzi 9,000 wamenufaika na scholarship hii.”
Katika kipindi hiki, tumes witnessing maendeleo makubwa katika miundombinu ya elimu kama vile vyumba vya madarasa, shule mpya, vyuo vya ufundi, na vyuo vikuu. Hadi sasa, tumeona ujenzi wa kampasi mpya 16 za vyuo vikuu na vyuo vya ufundi katika mikoa mbalimbali.”
Kwa upande wa mikopo ya elimu ya juu, jumla ya wanafunzi 830,000 wamenufaika na mikopo ya shahada, ikiwa ni gharama ya TZS Trilioni 8.2.”
Katika shule za sekondari, vyumba vya madarasa vimeongezeka kutoka 17,000 mwaka 2020 hadi 48,473 mwaka 2024. Idadi ya shule mpya za sekondari imeongezeka kutoka 5,280 mwaka 2020 hadi 5,807 mwaka 2024, huku idadi ya wanafunzi ikiongezeka kutoka 2,273,003 hadi 2,695,750.”
Tukiangazia takwimu, tunaona kasi kubwa ya uwekezaji na utekelezaji. Uwekezaji huu unajikita katika ngazi za awali, msingi, sekondari, na elimu ya juu, kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata elimu bora.”
KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
Kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi kazi,serikali imeratibu na kuunganisha Watanzania 1,877 (Wanaume – 437, Wanawake – 1,440) na fursa za ajira nje ya nchi;
Serikali imeratibu na kuunganisha Wahitimu 811 na fursa za mafunzo ya uzoefu wa kazi. Utekelezaji huu ni sawa na asilimia 54.06 ya lengo la kuunganisha wahitimu 1,500;
Vile vile serikali imezindua Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi kwa Watu Wenye Ualbino na Mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi kwa Watu wenye Ulemavu unalenga kupunguzu unyanyapaa, kuboresha ulinzi wa Watu wenye Ualbino na kuendeleza usawa wa kijamii katika upatikanaji wa huduma na fursa. Vilevile Mkakati Teknolojia Saidizi kwa Watu wenye Ulemavu utaweza kuweka mifumo imara na endelevu, taratibu na miundo ya utoaji wa huduma kwa ajili ya utoaji wa vifaa saidizi na huduma ambata fikivu kwa wote, zinazolingana , salama, zenye ufanisi na nafuu kwa watu wanaohitaji Teknolojia Saidizi.
Serikali imeendelea kulipa watumishi wanaostaafu kuanzia Julai 2024 kwa kutumia Kanuni mpya ya mafao ambapo watumishi 5,174 waliostaafu kuanzia Julai 2024 hadi Desemba 2024 wamelipwa mafao yao kiasi cha shilingi bilioni 76.85. Hivyo basi, jumla ya wanufaika 23,243 wamelipwa mafao kwa kutumia Kanuni mpya ya malipo ya mkupuo wa asilimia 40 na35 na jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 186.23 kimetumika kulipa wastaafu hao.
VIWANDA NA BIASHARA
Chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, sekta ya viwanda na biashara imepiga hatua kubwa katika miaka minne iliyopita. Serikali imeunda mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji na kuimarisha uchumi wa Tanzania.”
Tanzania sasa ina viwanda 14 vya magari, ikiwemo viwanda viwili vya kuunganisha magari: GF Trucks and Equipment Ltd huko Kibaha na Saturn Corporation Limited huko Kigamboni. Viwanda hivi vinachangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya ujenzi wa magari nchini.
Tanzania pia ina viwanda vitatu vya vioo, ikiwemo Kioo Ltd, Salehbhai Glass Industries Ltd, na Sapphire Float Glass Company Limited. Pamoja na viwanda 14 vya saruji, sekta ya ujenzi na ustawi wa miundombinu imeimarishwa kwa kiasi kikubwa.”
Katika kipindi hiki, Wizara ya Viwanda na Biashara imefanikisha maonesho 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba). Kampuni 3,954 zilishiriki, na mauzo ya papo kwa papo yalifikia Shilingi Bilioni 3.62, akionyesha nguvu ya uchumi wa Tanzania katika soko la kimataifa.”
Viwanda hivi sio tu vinavyozalisha bidhaa za kiwango cha juu, bali pia vinajenga ajira na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.”
Kwa pamoja, mafanikio haya yanaonesha juhudi za serikali ya Rais Samia kwa kuleta maendeleo endelevu katika sekta ya viwanda na biashara. Tanzania inaendelea mbele, kwa viwanda hai na biashara zinazokuwa.”
Haya yote ni mafanikio na juhudi za serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka minne katika kuhakiksha anaboresha sekta mbalimbali zinazohudumia wananchi wa Tanzania.