Kufuatia matukio ya mara kwa mara ya Wizi wa Mifugo katika Wilaya ya Rorya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mara Mary Daniel amewataka vijana wilayani Rorya kuacha kuvinyoshea vidole vyombo vya Dola kukomesha Vitendo hivyo badala yake nawao kuwa mstari wambele kuwaweka wazi wanaoishiriki katika matukio hayo
Mary ametoa kauli hiyo Wakati akizungumza na Vijana na makundi mbalimbali wakiwemo bodaboda,mama ntilie pamoja na wavuvi ambapo amesema ili kuhakikisha vitendo hivyo vinakoma vijana wanawajibu wakuvisaidia vyombo vya Usalama katika mapambano hayo
“Usitegemee hivi vitendo vinafanyika nyinyi hamjui au Wanaofanya hatuwajui tunatakiwa kuwataja wanahusika tunawajua lakini pia muweke ulinzi shirikishi hatutarajii kusikia nanyinyi mnalalamika”Alisema Mary Daniel Mwenyekiti wa UVCCM Mara.
Baadhi ya vijana wamesema sikwamba hawashiriki katika kukabiliana na matukio hayo ya Wizi lakini wamekuwa wakiwakamata wezi wanapowafikisha kwenye vyombo vya Dola wanaachiwa huru.