TANZANIA itaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya haki ya mtumiaji duniani ifikapo Machi 15 mwaka huu ambapo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mjini Morogoro.
Akizungumza leo Machi, 10 2025 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jukwaa la watumiaji Tanzania (TCF) Daud Daudi amesema maadhimisho hayo yanakusudia kuhamasisha matumizi salama na endelevu ya rasilimali na yatatoa jukwaa la majadiliano kati ya watumiaji ,watoa huduma,na wadau wa maendeleo.
Amesema katika maadhimisho hayo yatatoa firsa ya kujifunza kuhusu haki za mtumiaji na jinsi ya kutumia ya kutumia huduma salama.
“Hii ni fursa ya kipekee kwa wananchi kupata elimu kuhusu haki zao, huku Serikali na wadau wa sekta husika wakihimizwa kuhakikisha huduma bora na za haki zinapatikana kwa wote,”amesema.
Aidha amesema maadhimisho yanaadhimishwa kimataifa kwa lengo la kulinda haki za watumiaji na kuhimiza matumiza matumizi salama na endelevu ya huduma.
Vilevile amesema mtumaiji anapaswa kuw ana nguvu ya kufanya maamuzi sahihi kwa kupata huduma salama ,nafuu ,na endelevu na kila mtu ana haki ya kuishi katika jamii inayowajibika kulinda mazibgira na rasilimali kwa vizazi vijavyo.
Amesema matumizi salama ya huduma katika sekta za nishati .mawasiliano na usafiri wa anga na nchi kavu,ambapo Serikali ina lenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ay kupikia,hivyo wasibaki nyuma katika mabadiliko kutumia nishati safi sit u kwa faida ya leo bali kwa afya na ustawi wa kesho.
Akizungumzia mawasiliano ,usalama wa watumiaji mtandaoni ni ajenda muhimu mwaka huu TCF itahimiza ulinzi wa faragha na matumizi salama ya huduma za kidijitali na usalma katika sekta ya usafiri wa anga na nchi kavu utaangazwa ili kuhakikisha huduma bora kwa watumiaji .
Ametoa wito kwa vyombo vya habari kushirikaina katika kuhamasisha elimu kwa watumiaji kote nchini ambapo wakihamasisha matumizi endelevu leo wanajenga msigi wa kesho bora kwa jamii na uwajibikaji wa pamoja ni nyenzo ya kuleta maendeleo endelevu.
Nao wadau wa kutetea watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa Shrika lisilo la kiserikali la The foundation for civil society (FCS) TCAA –CCC, EWURA-CCC na TCRA –CCC walisema mwananchi ni mdau mzuri wa maendeleo hivyo wanapaswa kutatuliwa changamboto mbalimbali zinazowakabili na wapi atapata huduma na wakati gani .
Maadhimisho hayo yanaandaliwa na jukwaa la watumiaji Tanzania (TCF) linalojumuisha mabaraza ya kutetea watumaiji wa huduma zinazodhibitiwa ambayo ni LATRA –CCC ,TCAA-CCC ,EWURA-CCC na TCRA –CCC na Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation for Civil Society (FCS).