NA VICTOR MASANGU, PWANI
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewataka watendaji wa Kata pamoja na wakuu wa usalaam wa Wilaya zote ndani ya Mkoa huo kuongeza juhudi za utendaji kazi hasa kwa kuwahudumia wananchi kwenye maeneo yao kwani kufanya hivyo ni kutekeleza agizo la Rais wa nchi ambae amekuwa kisisitiza kuwa kipaumbele chake ni kuondoa kero kwa jamii
Kunenge ameyasema hayo leo Jumatatu Machi 10,2025 wakati wa mafunzo ya uraia na utawala bora yaliyofanyika Mjini Kibaha chini ya Wizara ya katiba na sheria lengo likiwa ni kuwajengea uwezo watumishi hao juu ya kuimarisha utendaji kazi wao
“Sisi sote tunamwakilisha mheshimiwa Rais wetu na kipaumbele chake ni kuondoa kero kwa wananchi wake hivyo tusipotekelza majukumu yetu sawsawa tutakuwa tuna muangusha jambo ambalo halitakiwi”amesema
Amewataka watendaji hao kuyatumia mafunzo hayo kwa kuboresha utendaji wao na kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao jambo litakaloleta faida kulingana an malengo ya serikali
“Mkiyatumia vizuri mafunzo haya italeta maana lakini kama mtayapuuza itakuwa hasara kwa muda uliotumika na hata gharama zilizotumika hivyo ni vema mkayafanyie kazi ili yalete tija” amesema.
Kwa upande wake Mrakibu msaidizi wa Polisi Nicolaus Mhagama amewataka watendaji wa kata kuzingatia kanuni na sheria zilizopo pindi wanapowahudumia waannchi ili kuepusha migogoro isiyokuwa na ulazima
“Sasa hivi serikali imewaongezea nguvu kwa kuwaletea Polisi Kata hao ni watu muhimu ambao mnaweza kushirikiana nao huko kwa kuimarisha usalama” amesema
Mratibu wa mafunzo hayo kutoka wizara ya katiba na sheria wakili Prosper Kisinini amesema kuwa serikali imeona umuhimu wa kuwapa mafunzo hayo watendaji wa ngazi mbalimbali lengo likiwa ni kuimarisha utoaji wa huduma kwa jamii.


