Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akifunga Kikaokazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, kikao hicho kiliwashirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Sehemu ya kikaokazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, kikao hicho kiliwashirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Makamishna Wasaidizi wa Idara ya Bajeti, Wizara ya Fedha, Bi. Bahati Mgongolwa (kushoto), Bi. Vicky Jengo na Bw. Andambike Mololo, wakifuatilia kwa karibu Kikao cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, kikao hicho kiliwashirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na maafisa bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoa wa Ruvuma, Bw. Jumanne Mwankhoo, akitoa neno kwa niaba ya washiriki wa Kikao cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, wakati wa kufunga kikaokazi hicho ambacho kiliwashirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na maafisa bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu – TAMISEMI, Bi. Susana Nyarubawa, akichangia mada katika Kikaokazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, Jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa Kikao cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, wakifuatilia mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa katika kikaokazi hicho ambacho kiliwashirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha,Dodoma).
………….
Na Scola Malinga, WF, Dodoma
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, amewasisitiza Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Bajeti wa Mikoa kuandaa Mpango wa Bajeti wa Mwaka 2025/2026 wenye tija.
Ametoa msisitizo huo Jijini Dodoma, wakati akihitimisha kikaokazi cha siku mbili cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26.
Kikao hicho kiliwaleta pamoja wadau wa sekta husika ili kuainisha na kuibua maeneo ambayo mafungu yanaweza kushirikiana na kuleta ufanisi katika uandaaji na utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2025/26.
Uchambuzi huo unalenga kuhakikisha uratibu wa shughuli za Serikali Kisekta unaboreshwa ili kuongeza ushirikiano na nguvu ya pamoja (Synergies) katika utekelezaji wa mipango kati ya Sekta zinazotegemeana.