Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg.Kaspar Mmuya amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Ndg.Shaban Millao kwa kufanya maamuzi ya haraka ya kumgharamia Mwanafunzi aliyekuwa anasumbuliwa na uvimbe katika mkono.
Ras Mmuya ameeleza kuwa Kondoa Dc imepata Mkurugenzi bora kwani kitendo cha yeye kutoa fedha zake mfukoni na kugharamia matibabu hili ni jambo zuri na la kuigwa katika jamii
Ras Mmuya ameendelea kwa kusema kuwa kitendo cha mwanafunzi huyo kumtembelea ofisini kwake ni upendo wa hali ya juu na hivyo taarifa atazifikisha kwa Mkuu wa Mkoa na siku za mbeleni watakuja Kondoa kujua hali ya mwanafunzi huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Millao ameeleza kuwa suala la kijana huyo pindi alipofikishiwa mezani kwake ilimkosesha raha na akaamua kugharamia matibabu yake,kwani hata lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha watoto wote wanapatiwa elimu ndiyo maana aliamua kulibeba suala hilo ili mwanafunzi aendelee na masomo kwani uvimbe ule ulimfanya ashindwe kuandika darasani.
Hali ya Mwanafunzi Abilayi Iddi kwa sasa imeimarika ikiwa ni baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Jijini Dodoma.