Na Rahma Khamis Maelezo
Kamishna Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Juma Haji Ussi amewataka wakaazi wa Wilaya ya Kati kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura linalotarajiwa kuanza Mach 8
Wito huo ameutoa Skuli ya Fumba Wilaya ya Magharibi B’ wakati akitembelea vituo vya kuandikisha daftari la wapiga kura ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kukagua vituo hivyo
Amesema kwa mujibu wa taarifa wanazozipata kupitia vituo hivyo zoezi linafanyika kwa amani na utulivu hakuna tatizo lolote na kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa kwenye daftari hilo la wapiga kura amepata haki yake ikiwa ni maandalizi ya kupiga kura
Wakuu wa Vituo vya uandikisha daftari hilo wamesema kuwa zoezi linaendelea vizuri changamoto zilizopo ni ndogo ndogo kwenye mashine za kusomea vidole ambazo wameweza kuzitatua na kuendelea kufanya kazi.
Nao wananchi waliofika kuandikishwa katika daftari hilo wamesema kuwa kujiandikisha ni haki ya msingi kwani unaweza kufanya maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi bila ya kubugudhiwa .
Aidha wamewaomba wananchi wenzao ambao bado hawajajiandikisha katika daftari la wapiga kura kujitokeza ili kupata nafasi ya kupiga kura unapofika uchaguzi.
Katika ziara hiyo vituo mbalimbali vilitembelewa ikiwemo Fumba, Nyamazi, Maungani Kisauni Bweleo na Dimani.