Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Dokta Stagomena Tax akizungumza kwenye kongamano hilo mkoani Arusha leo.



Wadau mbalimbali wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kongamano hilo mkoani Arusha leo
……..
Happy Lazaro, Arusha .
Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Dokta Stagomena Tax amewataka wanawake kuhakikisha wanazitumia ipasavyo fursa mbalimbali wanazokuwa nazo ikiwemo za uongozi pamoja na kulinda haki na ustawi wa jinsia zote.
Dkt Stagomena ameyasema hayo leo mkoani Arusha alipokuwa mgeni rasmi katika kongamano la wanawake kanda ya Kaskazini kuelekea siku ya wanawake duniani 2025 ,ushiriki wa wanawake katika utalii na maliasili, miaka 30 ya azimio la Beijing.
Amesema kuwa zipo changamoto kwa pande zote na sio kwa watoto tu hivyo nguvu zaidi lazima ziongezwe katika kuhakikisha haki na isawa unapatikana kwa watu wote .
Aidha ameongeza kuwa ,kumekuwepo na changamoto ya ukosefu wa fursa sawa za kiuchumi ambayo hupelekea wao kufanya kazi kwenye mazingira ya chini.
Amewataka wanawake kuzitumia ipasavyo fursa za kiuchumi pindi wanapopewa fursa hizo wahakikishe wanazitendea haki kama ambavyo Rais Samia anavyofanya ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake.
“nataka kuona wanawake wananufaika ipasavyo na fursa mbalimbali za kiuchumi pamoja na kuchangamkia nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi zote kwani wana mchango mkubwa sana katika jamii.”amesema .
Kwa upande wake Naibu waziri wizara ya maendeleo ya jamii ,jinsia ,wanawake na makundi maalum Mwanaidi Ally Hamis amesema kuwa,katika kongamano hilo wataweza kujadili mchango wa sekta ya maliasili na utalii kwa wanawake kwani wanawake sasa hivi wamekuwa mstari wa mbele katika kumuunga Rais Samia mkono kwenye swala ya utalii.
Aidha amewataka wanawake kuhakikisha wanalinda jamii zetu sambamba na kutenga muda kwa ajili ya watoto wetu kuhakikisha vitendo vya ukatili vinaisha kabisa.
Katika kongamano hilo Tafiti 16 zitajadiiwa ambazo zinalenga kuwajengea uwezo wanawake katika maeneo mbali mbali yakiwemo ya uongozi utalii na fursa zilizopo .
Kwa upande wake Dkt Bakari George Mkuu wa Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru amesema kuwa ,wanahakikisha wanashirikiana katika kuhamasisha wanawake wanachangamkia fursa mbalimbali zikiwemo za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi .
Naye Mmoja wa wanawake katika kongamano hilo,Tausi Mbalamwezi amesema kuwa kuelekea kilele cha siku ya wanawake watapata fursa ya kujadili maswala mbalimbali ikiwemo ya uhamasishaji kuhusu utalii kwani sasa hivi utalii ndio kila kitu katika mazingira yetu.
“Kila mmoja anaona namna ambavyo Rais Samia anavyohamasisha swala zima la.nishati safi kwa kutoa magesi kwa wananchi lengo likiwa ni kutunza mazingira katika maeneo yetu na kuacha kuharibi mazingira. “amesema .
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Wanawake na wasichana 2025 tuimarishe haki ,usawa na uwezeshaji.”