VICTOR MASANGU, KIBAHA
Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha kwa pamoja imeridhishwa na miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo maji, elimu, afya miundombinu ya barabarara pamoja na hudumu nyingine za maendeleo iliyotekelzwa kwa kipindi cha kuanzia Julai 2024 hadi Disemba mwaka 2024.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu cha Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Julai 2024 hadi Desemba 2024 kilichohudhuria na viongozi wa chama pamoja na serikali kwa ajili namna ya ilani ya chama ilivyotelekezwa katika miradi ya mbali mbali ya maendeleo.
Nyamka amesema kwamba wameweza kupita katika maeneo mbali mbali kwa ajili ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ambapo kwa kauli moja yameipitisha kutokana na kuona kazi nzuri ambayo yameifanya katika utekelezaji huo wa miradi ambayo itaweza kuwa mkombozi mkubwa katika kuwasaidia kwa kiais kikubwa wananchi kuweza kupata huduma kwa urahisi katika mahitaji mbali mbali.
Aidha Nyamka amebaisha kwamba katika kikao hicho wamewez kumpongeza kwa dhati Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John kwa kuweza kupambana na kuweza kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwani miradi mbali mbali imeweza kutekelezwa.
Aidha kikao hicho kimempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kibaha mjini Dkt. Rogers Shemwelekwa kwa kuwekakuweka mikakati mizuri ambayo imeweza kuongeza chachu zaidi katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ya ndani ikiwemo sambamba na kusimamia maslahi ya watumishi wake.
Pia Mwenyekiti huyo hakusita kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe:Silvestry Koka kwa kutekeleza majukumu yaoke ipasavyo ya kuwatumikia wananchi ikiwemo suala zima la kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo hali amabayo imechangia kwa kiais kikubwa kuweza kuleta chachu ya maendeleo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema kwamba ameweza kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo kwani miradi mingi katika sekta mbali mbali ya maji, afya, elimu, miundombinu ya barabara pamoja na mambo mengine ya huduma za kijamii imeweza kutekelezeka kwa kiwango kikubwa.
Kwa upande wake Katibu wa chama caha mapinduzi (CCM) Issack Kaleiya amesema kwamba miradi hiyo amabyo walipita kwa ajili ya kukagua ni moja ya utekeelzaji wa ilani ya chama na kwamba itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kutatua kero na changamoto mbali mbali za wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amebainisha kwamba katika Halmashauri ya Kibaha mji Ilani ya chama imeweza kutekelezwa katika miradi mbali mbali ya maendeleoa na kumshukuru kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Sauluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha ambazo zimekwenda kutekeleza miradi ya maendeleo.



