Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameshiriki Ibada ya Jumatano ya Majivu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Osterbay Jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Machi 2025. Ibada ya Jumatano ya Majivu ni mwanzo wa kipindi cha Kwaresma ambacho hutumika na waumini wa dini ya Kikristo kwaajili ya mfungo.