Meneja wakala ya Barabara Tanroads Mkoani mara imeitaja Wilaya ya Bunda kuwa ndio Kinara kwa Wizi w Taa za barabarani ambapo ameziomba mamlaka kusaidia kuchukua hatua za haraka kukomesha vitendo hivyo.
Kauli hiyo ameitoa katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoani Mara ambapo Alisema pamoja na mikakati mikubwa inayofanywa na Serikali ya kuboresha maeneo ya sante Vijijin ikiwemo kuweka taa za barabarani kwaajili ya kusaidia kufanya Biashara hususan nyakati za usiku lakini bado ipo changamoto kubwa ya Wizi wa Taa hizo.
Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijiji Mwita Waitara Alishauriwa kuondolewa Taa katika maeneo yote yanayaoshiriki Wizi huku akibainisha kupewa Maeneo ya Tarime Vijijin.
Mkuu wa Mkoa wa mara Kanali Evans Mtambi ameviangiza vyombo vya ulinzi na Usalama kuchukua hatua Kali za kufanya msako ili kuwabaini Wanaofanya vitendo hivyo.