Katika kuunga jitihada za uhifadhi na kurejea huduma kwa jamii inayozungukwa na mapori ya akiba ya Grumeti na Ikorongo kampuni ya Grumeti Reserves imechangia vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi Milioni 12 kwa Mitaa Mitatu ya Bunda Mji ambayo ni Mihale,nyamatoke,na Bukore.
Akizungumza katika hafla hiyo Meneja Idara ya Mahusiano Grumeti Fund David mwakipesile kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Grumeti Reserves Alisema vifaa hivyo vilitolewa kwa makubaliano ya viongozi wa Vijiji na kampuni ya Grumeti Reserves kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi wa Bunda mji ili kuhakikisha kuchangia shughuli za maendeleo katika mitaa hiyo ikiwepo kupunguza changamoto ya madarasa mashuleni hususani kwenye maeneo ambayo yanachangamoto kubwa ya wanafunzi kutembea umebali mrefu.
“Wananchi mnawajibu wakuhakikisha mnalinda wanyama hawa ikiwemo kujiepusha na vitendo vya Ujangili pamoja na uharifu wa Mazingira niwaombe Sana Sisi kama Grumeti tutahakikisha mahusiano Baina yetu nanyinyi wananchi yanakuwa karibu Zaidi maana wote tunategemeana ndio maana tumekuja na vifaa hivyo” Alisema David Mwakipesile.
Baadhi ya wananchi katika Vijiji hivyo wameipongeza kampuni hiyo kwa namna inavyotekeleza Miradi katika maeneo ya wananchi kwa kufata makubaliano waliyowekeana ya kuchangia Miradi lengwa
Huku Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt Vincent Anney Naano aliwataka wananchi hao kuthaminini na kuvilinda vifaa vinavyotolewa kwaajili ya Maendeleo yao.