Mwanamuziki Maarufu wa Muziki wa Injili, Patricia Kanya akiwa katika pozi.
……………………
Na Dotto Mwaibale, Arusha
WANAMUZIKI Wanawake wanaoimba nyimbo za injili Mkoa wa Arusha wamejipanga sawasawa kunogesha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa kuimba nyimbo bora ukiwepo wa maadhimisho hayo.
Mwanamuziki Maarufu wa nyimbo za injili nchini, Patricia Kanya ambaye ameshiriki katika wimbo huo maalum wa siku hiyo muhimu kwa wanawake akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Machi 1, 2025 alisema siku hiyo Arusha itasimama na kupata
burudani ya aina yake.
“ Wanawake waimbaji wa nyimbo za injili Mkoa wa Arusha tumejipanga vilivyo kutoa nyimbo kadhaa tulizo ziandaa ukiwepo wimbo maalumu kwa ajili ya siku yetu hiyo,” alisema Kanya.
Alisema baadhi ya nyimbo hizo zina maudhui ya kuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muunguno wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta mbalimbali na kuhamasisha wananchi
kuungamkono jitihada hizo.
“ Tayari tumekwisha rekodi baadhi ya nyimbo ambazo zinahamasisha kudumisha Amani na Utulivu wa nchi
na kuendelea kudumisha ushirikiano hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2025,” alisema Kanya.
Alisema Wanawake wote wa Mkoa wa Arusha chini ya Mkuu wao wa Mkoa, Paul Mkonda hawata poa kumsemea Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo makubwa aliyoyafanya ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wa Tanzania na kueleza kwamba wimbo wao huo
maalumu utakuwa na kaulimbiu ya maadhimisho ya siku hiyo mahususi kwa ajili ya wanawake duniani 2025.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abed jijini Arusha ambapo kilele chake ni Machi 8, 2025 na mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.