Mkuu wa mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere wakati akifungua kikao Cha 43 cha bodi ya barabara mkoa wa Rukwa
Meneja wa TARURA mkoa wa Rukwa Chacha Msendi wakati akizungumza na waandishi wa habari
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Aesh Halfan Hilary akizungumza na waandishi wa habari katika kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukile akifafanua kuhusu utekelezaji wa kazi za barabara za TARURA
Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao Cha 43 cha bodi ya barabara mkoa wa Rukwa.
………………
Na
Neema Mtuka ,Sumbawanga
Rukwa :Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Charles Nyerere amewataka wakandarasi wote katika halmashauri zote za mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanasimamia miradi kwa weredi mkubwa na kuilinda miundombinu ya barabara pindi wanapofanya kazi zao.
Makongoro amesema hayo katika kikao cha 43 cha bodi ya barabara kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa RDC na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wadau wa barabara.
Aidha Makongoro amewataka TANROADS na TARURA kulifanyia kazi suala la uharibifu wa miundo mbinu ya barabara kwa kutumia sheria zilizopo.
Kwa upande wake meneja wa TARURA mkoa wa Rukwa Chacha Msendi wakati akitoa wasilisho la utekelezaji wa kazi za barabara za wilaya kwa mwaka 2023/2024 na 2024 /2025 pamoja na maoteo ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 amesema kuchelewa kwa malipo ya miradi ,uvamizi wa hifadhi za barabara na usafirishaji wa mifugo barabarani unakwamisha juhudi za kufika kusiko fikika.
Msendi amesema wapo tayari kwa ajili ya kufanya kazi na kusimamia miradi yote inayotekelezwa na TARURA na watahakikisha wanawashirikisha wananchi na kuwapa elimu ili na wao wailinde miundombinu inayopita kwenye maeneo yao .
Naye kaimu meneja wa Tanroads mkoa wa rukwa amewataka wananchi kuacha tabia ya kufanya shughuli za kibanaadamu kando ya barabara ikiwemo wakulima wa mpunga na baadhi ya wafugaji kufanya usafirishaji wa mifugo barabarani ambapo wanasababisha uharibifu mkubwa katika miundombinu hiyo.
Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Aesh Halfani Hirary amewataka Tanroads na wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA kuhakikisha wanawalipa wananchi fidia kabla ya kuwaondoa katika maeneo yao wakidai kupisha ujenzi wa barabara na kuepusha migogoro kati yao na wananchi kwa kuweka alama X bila malipo na wao kutotumia maeneo hayo kwa zaidi ya miaka 15 na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla .
Wakizungumzia suala hilo baadhi ya wananchi akiwemo Said Azizi amesema nyumba yake iliwekewa alama X akidaiwa kuvamia eneo la barabara mapaka sasa ni miaka 15 hawajawahi kulipwa fidia na kuendeleza maeneo yao .
“Tunawaomba Tanroads kabla ya kuja kuweka alama wawe wanatoa elimu kwanza kwa wananchi ili tuwe na uelewa wa kutosha kitendo walichokifanya cha kuweka nyumba zetu X na kutukataza kusiendeleze maeneo yetu ni kuturudisha nyuma na kudididmiza uchumi wa nchi”Amesema Azizi.
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukile akichangia kuhusu taarifa ya utekelezaji wa kazi za barabara za Tanroads amesema kiasi cha pesa kilichosalia katika bajeti iliyopita ni bora kipelekwe kuendeleza barabara inayounganisha wilaya ya sumbawanga na Kalambo kwa lengo la kufungua wilaya hizo na nchi jirani ya Zambia na kujiingizia kipato.