Mwandishi Mwandamizi wa Azam Media Ltd, Augustine Mgendi, ameibuka mshindi wa nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoka Mkoa wa Mara.
Mgendi ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 5 kati ya 9 zilizopigwa, huku kura moja ikiharibika na hivyo kura halali kuwa tisa.
Uchaguzi huo wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM) umefanyika leo, Machi 1, 2025, katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Katika uchaguzi huo, Mussa Nyamandege, aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti, amethibitishwa kuwa Mwenyekiti wa FAM, huku wajumbe wa mkutano wakihudhuria na kushiriki uchaguzi huo.
Aidha, baada ya uchaguzi huo, Mwenyekiti mteule wa FAM, Mussa Nyamandege, amemteua Haroub Salum kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.
Katika kinyang’anyiro cha ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, Mgendi aliwapiku wagombea wenzake, Revocatus Kuboja aliyepata kura 4, na Mecksedek Mtobesha ambaye hakupata kura yoyote.