Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Kaspar Mmuya, amesema kuwa programu ya Lipa kwa Matokeo (P4R) imeleta mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma za kijamii mkoani humo. Alisema mafanikio ya programu hiyo yanachochea uwekezaji na kuvutia wakazi zaidi katika makao makuu ya nchi.
Bw. Mmuya alieleza kuwa matokeo ya P4R ni chanya, na bado kuna uhitaji mkubwa wa kuendeleza programu hiyo kwani jamii inakua na mahitaji yake yanaongezeka kila siku. Aliongeza kuwa elimu kuhusu mabadiliko ya tabianchi na athari zake inatolewa kwa wananchi, hadi ngazi za chini, kwa kuwa huduma za maji safi ni hitaji muhimu kwa zaidi ya wakazi milioni 3.5 wa Dodoma wanaonufaika na P4R.
Miongoni mwa mafanikio ya P4R katika Mkoa wa Dodoma ni pamoja na:
Kuimarisha elimu – imeongeza ufaulu wa wanafunzi na kupunguza utoro shuleni.
Kuboresha huduma za afya – wananchi wanapata huduma bora za afya.
Upatikanaji wa maji safi – huduma ya maji imeimarishwa kwa wananchi wengi zaidi.
Bw. Mmuya alihitimisha kwa kusisitiza kuwa P4R ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya Dodoma, kwani inaendelea kuleta mageuzi katika sekta mbalimbali za kijamii.