Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akichangia hoja katika majadiliano katika sehemu ya pili ya Mkutano wa 16 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Hifadhi ya Bioanuai unaofanyika jijini Roma, Italia.
…………..
Serikali ya Tanzania imesema kuwa ni wakati muafaka sasa wa kuanzisha Chombo maalumu cha kuwezesha upatikanaji wa fedha za kuhifadhi bioanuai kama ilivyoelekezwa katika ibara ya 21 ya Mkataba wa Hifadhi ya Bioanuai.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati akichangia hoja katika majadiliano katika sehemu ya pili ya Mkutano wa 16 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Hifadhi ya Bioanuai unaofanyika jijini Roma, Italia.
Mhandisi Luhemeja ambae anaongoza Ujumbe wa Tanzania amesema kuwa imeelekezwa katika Ibara ya 21 ya Mkataba wa Hifadhi ya Bioanuai amesema ni vyema pia kufanya tathmini ya Mifuko ya Fedha iliyopo ili kuiimarisha katika kuwezesha masuala ya uhifadhi wa bioanuai duniani.