Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba akieleza jinsi mkoa anaouongoza utakavyotoa ushirikiano katika kufanikisha miradi mbalimbali ya Lipa kwa Matokeo (P4R) katika huduma ya maji, elimu na afya.
Amesema ni muhimu jamii kushirikishwa na kuelewa faida za miradi hiyo, pamoja na viongozi ili kuwa na uendelevu imara wa miradi kama inavyofanyika hivi sasa. Amesema mkoa wa Iringa ni moja kati ya mikoa inayofanya vizuri na wako tayari kwa ushirikiano zaidi.
Programu ya P4R katika mkoa huo imewezesha upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 72 hadi asilimia 79, na miradi katika maeneo mbalimbali bado inaendelea.
Mrejesho kuhusu utekelezaji wa programu ya P4R umewasilishwa kwa Mhe. Serukamba na mwakilishi wa Benki ya Dunia kutoka Marekani Bi. Toyoko Kodama ambaye ndio kiongozi katika kazi hiyo na amesisitiza ushirikishwaji wa jamii ni moja ya jambo muhimu katika kufanikisha uendelevu wa miradi inayotekelezwa ili iendelee kuwa bora kwa kuwafikia wanufaika wengi katika jamii.