Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek nchini Namibia leo tarehe 27 Februari 2025. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maombolezo ya Kitaifa na Ibada ya kumuaga aliyekuwa Rais wa kwanza wa Namibia hayati Dkt. Sam Nujoma itakayofanyika tarehe 28 Februari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Balozi wa Namibia nchini Tanzania Mhe. Balozi Lebbinus Tobias wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini
Windhoek nchini Namibia leo tarehe 27 Februari 2025. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maombolezo ya Kitaifa na Ibada ya kumuaga aliyekuwa Rais wa
kwanza wa Namibia hayati Dkt. Sam Nujoma itakayofanyika tarehe 28 Februari 2025.
……………..
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 27 Februari 2025 amewasili Jijini Windhoek nchini Namibia ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maombolezo ya Kitaifa na Ibada ya kumuaga aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Namibia hayati Dkt. Sam Nujoma.
Utoaji wa heshima za mwisho na Ibada ya kumuaga Kitaifa hayati Dkt. Nujoma itafanyika katika Uwanja wa Michezo wa Uhuru uliopo Jijini Windhoek tarehe 28 Februari 2025 na Mazishi yatafanyika katika eneo la Makaburi ya
Mashujaa yaliyopo katika Jiji la Windhoek nchini Namibia tarehe 01 Machi 2025.
Franco Singaile
Msaidizi wa Makamu wa Rais – Habari