Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) wakishangilia mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Bagamoyo (Makurunge) – Pangani – Tanga: sehemu ya Mkange – Pangani – Tanga (km 170.8) kwa kiwango cha lami pamoja na Daraja la Mto Pangani (m 525) na barabara unganishi (km 25) Mkoani Tanga, Februari 26, 2025.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Bagamoyo (Makurunge) – Pangani – Tanga: sehemu ya Mkange – Pangani – Tanga (km 170.8) kwa kiwango cha lami pamoja na Daraja la Mto Pangani (m 525) na barabara unganishi (km 25) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) Februari 26,2025, mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Bagamoyo (Makurunge)- Pangani-Tanga (km 256) sehemu ya
Mkange- Pangani- Tanga (km 170.8) pamoja na Daraja la Mto Pangani (m 525) iliyofanyika wilayani Pangani mkoani Tanga tarehe 26 Februari,2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa wilaya ya Pangani, Mkoani Tanga katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Bagamoyo (Makurunge)- Pangani-Tanga (km
256) sehemu ya Mkange- Pangani- Tanga (km 170.8) pamoja na Daraja la Mto Pangani (m 525) iliyofanyika wilayani Pangani mkoani Tanga tarehe 26 Februari,2025.
Muonekanao wa Daraja la muda linalotumika kupitisha vifaa kwa ajili ya ujenzi sambamba na ujenzi wa nguzo za Daraja la mto Pangani ukiendelea Wilayani Pangani Mkoani Tanga. (PICHA NA WU)
…………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuufungua na kuunganisha Mkoa wa Tanga na ushoroba wa Ukanda wa Pwani pamoja
na nchi jirani kiuchumi, kibiashara na kiutalii.
Rais Samia ameeleza hayo Wilayani Pangani, Mkoani Tanga tarehe 26 Februari, 2025 mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Bagamoyo – Pangani – Tanga (km 256): sehemu ya Mkange- Pangani-
Tanga (Km 170.8) kwa kiwango cha lami pamoja na Daraja la Pangani (m 525) na barabara unganishi (km 25).
"Barabara hii tunayoiunganisha inakwenda kuifungua Tanga kiutalii na kibiashara, maeneo kadhaa ya utalii sehemu za Tanga ambayo hayafikiki ambyo sasa kwa barabara hii ni rahisi kufikika kwani tutaweza kumtoa mtalii Saadani na kumpeleka maeneo mengine ya kufanya utalii ndani ya
Tanga", amesisitiza Rais Samia.
Rais, Dkt. Samia amesema kuwa barabara hiyo pamoja na Daraja la Pangani ni kiungo muhimu kati ya Bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mombasa na hivyo kutasaidia kuchochea uchumi wa Buluu.
Halikadhalika, barabara hiyo itawezesha wananchi kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo hususan Mihogo, nazi na mwani na hivyo itarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji hadi katika masoko mbalimbali ndani na
nje ya Mkoa wa Tanga.
Rais Samia ameongeza kuwa barabara hiyo ikikamilika itakuwa pia kiungo muhimu cha barabara za Ushoroba wa Kaskazini, Kati, Kusini na Magharibi na kuifanya kuwa kiungo kizuri cha Nchi za Kusini mwa Afrika
pamoja na Nchi za Maziwa Makuu.
Aidha, Rais Samia ameielekeza Wizara ya Ujenzi kukamilisha kipande cha barabara hiyo kilichobakia chenye urefu wa kilometa 8 ili kuunganisha hadi Pangani kutokea Tanga.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia imefanikisha kukamilisha ujenzi wa madaraja nane makubwa yakiwemo Daraja la Tanzanite ( Dar
es Salaam), Kitengule (Kagera) na Msingi (Singida) ambayo yana thamani ya Shilingi Bilioni 381.
Ameongeza kuwa Rais Dkt. Samia pia amesaidia kukamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa Kilometa 1,366 nchi nzima zenye thamani ya shilingi Trilioni 2.7 na huku barabara zenye urefu wa Kilometa 2,031 zipo
katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Kadhalika, Ulega ameeleza kuwa Rais Samia ameendeleza utekelezaji wa miradi mingine ya madaraja makubwa ikiwemo Daraja la Pangani (m 525) pamoja na barabara unganishi (Km 25) na kusisitiza kuwa daraja hilo
litakapokamilika litawekwa jumla ya taa 240 huku taa 200 zikiwekwa katika mji wa Pangani ili kuupendezesha mji huo.
Ulega amemhakikishia Rais, Dkt. Samia kuwa Wizara ya Ujenzi wataendelea kuwasimamia Wakandarasi wanaojenga miradi hiyo usiku na mchana ili kukamilika kwa viwango na kwa wakati.
Awali, akitoa taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi, Mohamed Besta amesema kuwa barabara ya Bagamoyo – Pangani – Tanga na Daraja la Pangani
unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.