Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Iringa Dkt. Linda Salekwa akikabidhi zawadi ya vazi la Kitenge kwa mwakilishi wa Benki ya Dunia kutoka nchini Marekani ambaye anaongoza timu ya wataalamu katika ukaguzi wa miradi ya maji katika programu la Lipa kwa Matokeo (P4R).
Dkt. Linda amesema kupitia P4R wilaya ya Mufindi imeimarisha huduma ya maji kwa wananchi katika makazi na maeneo ya huduma za umma, pia kuiwezesha Mufindi kuwa moja ya wilaya zinazofanya vizuri katika kutoa huduma kwa jamii. Pamoja na mengine timu hiyo imekagua uendelevu wa miradi na utunzaji wa vyanzo vya maji, ushiriki wa wananchi katika masuala mbalimbali ya miradi na jinsi wanavyoipokea na Serikali ilivyowazi katika kupokea mrejesho wa wananchi kuhusu huduma ya maji.