Bi. Toyoko kodama , mwakilishi wa Benki ya Dunia kutoka nchini Marekani, akijionea huduma ya maji ilivyoimarishwa kwa wananchi kupitia Programu ya Lipa kwa Matokeo (P4R) wilaya ya Kilolo, Iringa. Programu hiyo ambayo imeleta mabadiliko katika maeneo ya umma zikiwemo shule na zahanati ambapo imeimarisha kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji Kilolo kutoka wastani wa asilimia 64.8 mwaka 2019 hadi asilimia 78 hivi sasa. Tanzania ni moja ya nchi zilizofanya vizuri zaidi katika programu hiyo Duniani.
BENKI YA DUNIA WAKAGUA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA LIPA KWA MATOKEO KILOLO
