Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja akisaini
kitabu cha maombolezo alipowasili eneo la Makongo Jijini Dar es Salaam leo
Februari 22, 2025 kwa ajili ya kutoa pole na kuifariji familia ya aliyeshiriki
tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar
Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja akiifariji
familia ya aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika
na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael Mushi. Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye
amefariki dunia Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja akiwafariji
waombolezaji alipowasili eneo la Makongo Jijini Dar es Salaam leo Februari
22, 2025 kwa ajili ya kutoa pole na kuifariji familia ya aliyeshiriki tukio la
kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi.
Sifael Mushi ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja (katikati)
akiwa katika akiwa na Naibu Karibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan
Mitawi (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Muungano Dkt. Juma Mohamed Salum
na ndugu wa Marehemu Sifael Mushi aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo
wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar, wakati wa ibada ya fupi nyumbani
Makongo Juu Jijini Dar es Salaam leo Februari 22, 2025.
Sehemu ya waombolezaji nyumbani Makongo Juu Jijini Dar es Salaam
kufuatia kifo cha aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa
Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye amefariki dunia
Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja (katikati)
akiwa katika katika picha ya pamoja na familia ya Marehemu Sifael Mushi
aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na
Zanzibar, nyumbani Makongo Juu Jijini Dar es Salaam leo Februari 22, 2025.
………………
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja ametoa
wito kwa Watanzania kuendelea kudumisha na kutunza historia ya Muungano
kwa vizazi vya sasa na vijavyo ili kuwaenzi waasisi wake.
Ametoa wito huo wakati akizungumza na waombolezaji eneo la Makongo Juu
Jijini Dar es Salaam leo Februari 22, 2025 Jijini Dar es Salaam, alipofika kutoa
pole na kuifariji familia ya aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa
iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye
amefariki dunia Februari 20, 2025.
Akitoa salamu za Serikali, Mhandisi Luhemeja amesema Marehemu Sifael
alikuwa ni mtu muhimu katika historia ya Muungano wakati wa tukio la
kuchanganya udongo lililkofanyika Aprili 26, 1965 ikiwa ni mwaka mmoja
baada ya kuasisiwa kwa Muungano Aprili 26, 1964.
Akiifariji familia ya marehemu amesema pamoja na majonzi ya kumpoteza
mpendwa wao, ina bahati ya kupata mtu aliyeshuhudia Muungano ambao
umedumu hadi leo.
“Niwaombe tuudumishe Muungano kwani wengi wetu tumezaliwa baada ya
Muungano hivyo ni vyema tukaendelea kuitunza historia yake namna
alivyoshiriki katika tukio lile la kuchanganya udongo, ni nadra sana kumuona
Mtanzania mmoja ana picha ya Rais wa Awamu ya Sita, wa Awamu ya Tano,
Awamu ya Nne na Awamu ya Kwanza si jambo rahisi, lakini kwa Marehemu
Sifael tunalishuhudia,” amesema.
Marehemu Sifael ambaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania
walishiriki katika tukio la kuchanganga udongo wa Tanganyika na Zanzibar,
alifariki dunia katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam alipokuwa
akipatiwa matibabu.
Wengine walioshiriki katika tukio hilo na wametangulia mbele ya haki ni
Marehemu Hassanieli Mrema aliyefariki Mei 04, 2024, Marehemu Khadija
Abbas Rashid alifariki Agosti 22, 2023 na Marehemu Omar Hassan Mkele
alifariki Agosti 28, 2024.