Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe maalum kutoka Tume ya Mishahara ya nchini Zambia, leo tarehe 21 Februari, 2025 katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba Jijini, Dodoma.
Mkurugenzi wa Uratibu na Huduma za Ushauri wa Kisheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Neema Ringo , amesema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inazikaribisha taasisi mbalimabli za ndani na nje ya nchi kuja kujifunza na kupata ushauri wa kisheria kutoka katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
*”Sisi tunajisikia fahari na heshima kutembelewa na Tume ya Mishahara kutoka Zambia, nichukua nafasi hii kuzikaribisha taasisi nyingine zije zipate huduma zetu.”*
Ujumbe huo kutoka nchini Zambia umeongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Mishahara ya Zambia, Bw. Chembo Mbula ambae aliambatana na Mtendaji Mkuu wa TAZAMA nchini.