Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, Mhe. Temesgen Tiruneh amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajiwa kushiriki Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazolima Kahawa Afrika utakaofanyika Februari 21 na 22, 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataiafa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Baada ya kuwasili Mhe. Tiruhe amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam tarehe 21 Februari, 2025.
Mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha pamoja zaidi ya washiriki 1,000 kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kukuza uzalishaji wa zao hilo muhimu kwa uchumi wa Taifa.