
NA VICTOR MASANGU, PWANI
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Taifa Hamoud Juma (MNEC) kupitia wazazi katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 amezihimiza jumuiya zote za wazazi pamoja na wananchi kuhakikisha wanatumia siku zilizobaki kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ambalo linatarajiwa kufikia tamati Februari 19 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalumu kuhusiana na mwenendo mzima wa zoezi linaloendelea la uboreshaji wa daftari hilo amebainisha kwamba jumuiya za wazazi pamoja na wanachama wote wa CCM wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kujitokeza kwa wingi ikiwa pamoja na kuwahimiza wananchi wengine ambao walikuwa bado awajakwenda kujiandikisha kutokana na sababu mbali mbali.
Juma amesema kwamba kuna umuhimu mkubwa sana katika kushiriki kikamilifu katika daftari hilo ikiwa linakwenda sambamab na kuboresha taarifa za muhusika pamoja na kuwaandikisha watu wapya wengine ambao wameweza kutimiza umri wa miaka 18 na kuendeleoa amabpo hapo awali hawakuwemo kabisa katika daftari hilo.
“Nipende kuchukua fursa hii ya kuziimiza jumuiya zote za wazazi katika Mkoa wa Pwani pamoja na wanachama na viongozi wa kutumia fursa katika siku ambazo zimesalia katika kujiandikisha katika daftari hilo la kudmu kwani ni muhimu sana hasa kaatika kuelekea katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu kwa ajili ya kupataa viongozi wa nafasi mbali mbali ikiwemo Urais,wabunge pamoja na nafasi za wabunge mbali mbali,”alisema Mnec Juma.
Katika hatua nyingine amemewakata viongozi wa jumuiya mbali mbali hususan wazazi pamoja naa wanachama wote wa chama cha mapinduzi (CCM) kutofanya makosa hata kidogo na badala yake wanatakiwa wajipange mapema na kuwa na umoja na mshikamano wa kutosha katika kumpa kura nyingi za kishindo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,wabunge pamoja na madiwani wote wa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.