Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kumuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Februari 17, 2025. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknoloji, Profesa Adolf Mkenda, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Daniel Mushi, na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania , Profesa Hamisi Dihenga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Februari 17, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Nsekela (kulia) alipotembelea banda la maonesho la CRDB katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Februari 17, 2025. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji, Omary Kipanga na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu, Dkt. Bill Kiwia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kuingia kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Februari 17, 2025. Kushoto ni Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda na kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wananfunzi wa Elimu ya Juu wakimsikiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassn kwenye Maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Februari 17, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wakishiriki kuimba Wimbo wa Taifa katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Februari 17, 2025. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho hayo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Februari 17, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)