…………………….
Na Sixmund Begashe – Karatu
Wataalam wa Mimea vamizi katika maeneo yaliyohifadhiwa kutoka nchini Cuba wakiongonzwa na Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Tanzania, Mhe. Yordenis Despaigne Vera, wamewasili Wilayani Karatu Mkoani Arusha tayari kwa kuungana na wataalam wa Uhifadhi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ili kubadilishana uzoefu wa utatiti wa namna ya kukabiliana na changamoto ya Mimea Vamizi katika maeneo yaliyohifadhiwa kisheria kwa ustawi endelevu wa Ikolojia katika maeneo hayo.
Ziara ya wataalam hao hapa nchini imelenga kuungana na Wataalam wa Wizara ya Maliasili na Utalii, kutembelea hifadhi za Taifa na maeneo yaliyohifadhiwa ili kufanya tathmini ya kina ya changamoto ya mimea vamizi inayoharibu ikolojia na kuathiri malisho ya wanyama katika maeneo hayo hasusani Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Hifadhi ya Ngorongoro na Bonde la Ziwa Victoria.
Ziara hiyo ya kikazi iliyoratibiwa na Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Cuba, Mhe. Humphrey Polepole, ni matokeo ni chanya ya mahusiano yaliyotukika ya kidiplomasia kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu na Serikali ya Jamhuri ya Cuba.
Ujumbe wa wataalam hao uliwasili Jijini Dodoma kwa Treni ya mwendo kasi (SGR) na baadaye kuelekea Karatu kwa ndege ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)