Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amefanya mazungumzo na Prof. Jeffrey Sachs wa Chuo Kikuu cha Columbia cha nchini Marekani pembezoni mwa Mkutano wa 38 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika leo tarehe 16 Februari, 2025 kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia.
Mazungumzo yao yaliangazia namna Nchi za Afrika zinavyoweza kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi kwa kuwekeza katika rasilimali watu na ujenzi wa miundombinu.
Maeneo mengine waliyoongelea ni matumizi yenye tija ya mikopo na maendeleo ya sekta ya utalii.