Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) tarehe 13.02.2025 imetoa elimu kinga na ya udhibiti wa dawa za kulevya kwa watumishi 43 wa Taasisi mbalimbali wanaofanya kazi katika Kiwanja cha Ndege cha Arusha.
Washiriki wa mafunzo hayo walipewa mbinu kadhaa zinazotumiwa na wahalifu wa dawa za kulevya katika kuficha dawa hizo wakiwa wanapita katika maeneo ya viwanja vya ndege.
Washiriki wa Mafunzo hayo waliombwa kushirikiana na Mamlaka katika mapambano ya dawa za kulevya kwa kuwaumbua na kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kwa kupiga simu ya bure 119.



