NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka ameimiza jumuiya ya wanawake kuhakikisha kwamba wana kuwa na umoja na kushikamana na kuweka misingi imara na kumpa sapoti ya kutosha Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan aweze kushinda kwa kishindo kikubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mama Koka ameyasema hayo wakati wa kikao cha baraza la jumuiya ya wanawake Kibaha vijijini lililofanyika na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake kwa lengo la kujadili mambo mbali mbali ikiwemo suala zima la nkujiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Katika hatua nyingine amewahimiza wanawake wa jumuiya hiyo kuaanzia ngazi za matawi kuhakikisha kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambalo linatarajiwa kuanza kufanyika rasmi Februari 13 hadi 19 mwaka huu lengo ikiwa ni kupata fursa ya kupiga kura.

Kadhalika Mama Koka amempongeza kwa dhati dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha nyingi ambazo zimeweza kwenda kufanya mambo makubwa katika kutekeleza miradi mbali mbali ikiwemo afya, elimu, maji, pamoja na huduma za kijamii.
Kwa upande wake mjumbe wa Halmashauri ya chama cha mapinduzi CCM Taifa kupitia jumuiya ya wazazi (MNEC) Hamoud Juma amewataka wanawake kuunda kamati za ushindi kuanzia ngazi za matawi kwa lengo la kuweza kumpa kura nyingi Rais Samia Suluhu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.


