Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mkoani Geita Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa nia, dhamira na Upendo wake kwa wakazi wa Bukombe hasa kwa namna ambavyo amekuwa chachu ya maendeleo kwenye Jimbo la Bukombe.
“Nimshukuru sana Mhe. Rais kwa mapenzi makubwa na kwa maendeleo makubwa tuliyoyapata, Ninyi ni mashahidi kwa kazi kubwa nitakazozieleza hazitokani na jambo lolote isipokuwa yeye mwenyewe kuweka msisitizo kwenye kazi hizi na ndio maana Mkutano mkuu wa Chama uliamua kwa kauli moja kumteua moja kwa moja kuwa Mgombea kwenye uchaguzi ujao.” Amesema Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020-2025 kwenye Jimbo la Bukombe Mkoani Geita, leo Februari 08, 2024 mbele ya Mgeni rasmi Rais mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.