N๐ข ๐๐ข๐ฎ๐ฆ๐ด ๐๐ข๐ฎ๐ข๐ญ๐ข, ๐๐ง๐ช๐ด๐ข ๐๐ข๐ฃ๐ข๐ณ๐ช โ ๐๐ป๐ฆ๐จ๐ข ๐๐ซ๐ช.ย
Watanzania wameaswa kuacha dhana potofu kwamba vyakula vilivyoongezwa virutubisho lishe vinapunguza nguvu za kiume. Badala yake, wametakiwa kula vyakula hivyo kwa manufaa ya kiafya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha kinga ya mwili na kuulinda mwili na magonjwa mbalimbali.
Hayo yamebainika katika kikao cha lishe cha Halmashauri ya Mji wa Nzega kilichofanyika Jumatano, tarehe 29 Januari 2024.
โVirutubisho vinavyoongezwa kwenye vyakula kama vile unga, ngano, au mafuta ya kula havina madhara yoyote kwa afya ya uzazi au kupunguza nguvu za kiume. Badala yake, vinaimarisha afya za watumiaji,โ alisema Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, Dkt. Anna Chaduo.
Dkt. Chaduo aliongeza kuwa virutubisho lishe vinaongezwa kwenye vyakula ili kufidia upungufu wa vitamini na madini muhimu unaotokana na kupungua kwa rutuba ya udongo. Mbali na kuimarisha afya na kuongeza nguvu mwilini, virutubisho hivi pia hufanya ngozi ing’ae na kuwa na mwonekano mzuri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, Bw. Shomary Salim Mndolwa, aliagiza kuwepo na utaratibu wa kuhakikisha kuwa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vinavyosaga na kufungasha unga wa mahindi mjini Nzega vinaongeza virutubisho lishe kwa usahihi na kwa kuzingatia sheria za nchi.
โPamoja na kufuata sheria, ni muhimu pia kuwaelimisha wamiliki wa viwanda vya kusaga na kukoboa juu ya faida za kuongeza virutubisho lishe kwenye unga na bidhaa nyingine kwa manufaa ya afya bora kwa Watanzania,โ alisema Bw. Mndolwa.
Naye Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo, Bi. Caroline Fredy, alieleza kuwa kwa kipindi cha miezi sita iliyopita, viashiria vya mkataba wa lishe vimefikiwa kwa zaidi ya asilimia 90. Viashiria hivyo ni pamoja na utoaji wa matone ya Vitamini A kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano, ushauri wa lishe kwa wazazi na walezi, pamoja na matibabu kwa watoto wenye utapiamlo.
Viashiria vingine vilivyofikiwa ni usimamizi shirikishi wa shughuli za lishe mashuleni, ambapo shule zote za Halmashauri hiyo zinawapa watoto chakula wawapo shuleni. “Shule za msingi na sekondari zimeanzisha vilabu vya lishe, hivyo tunatarajia mabadiliko makubwa mwaka huu,” alisema Bi. Fredy.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai, alipongeza hatua zilizofikiwa na kuagiza kuwa changamoto zilizopo zishughulikiwe kwa haraka ili kuendana na kasi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuijenga Tanzania yenye afya bora na imara.