Na JAMES KAMALA, Afisa Habari – Nzega Mji.
Wakazi wa Kata ya Mwanzoli na maeneo jirani katika Halmashauri ya Mji wa Nzega, Mkoani Tabora, sasa wanapata huduma za Afya kwa urahisi baada ya kukamilika na kuanza kazi kwa Kituo cha Afya cha Kitengwe na kuwapunguzia gaharama na Mwendo mrefu wa kilometer 20 kufuata huduma hizo Hospitali ya Wilaya.
Kituo hicho, kilichogharimu jumla ya Shilingi Milioni 500, kilikamilika na kuanza kutoa huduma Mbalimbali kwa wagonjwa. Huduma zinazotolewa ni pamoja na matibabu ya wagonjwa wa nje (OPD), huduma za maabara, kuchangia damu (Blood donation) , kupumzisha wagonjwa, na huduma za afya ya baba, mama na mtoto ikiwemo Kliniki (RCH), Chanjo, Huduma za Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT), Tohara kinga (VMC), kuzalisha kawaida pamoja upasuaji wa akina mama wenye uzazi pingamizi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, Dkt. Anna Godwin Chaduo, alisema kuwa Huduma hizo za kisasa katika kituo cha Afya Kitengwe zimewezeshwa kufuatia serikali kutoa fedha jumla ya shilingi milioni 450 za ununuzi wa vifaa tiba kama vile Mashine za Kisasa za Ultrasounda, za kufulia, Dawa za usingizi na ganzi.
Alieleza kuwa fedha hizo pia zimetumika kununua kitanda cha kisasa cha upasuaji, mashine ya kugandisha damu kwa wgonjwa wakati wa kufanyiwa upasuaji. Vingine ni vifaa na mashine za kisasa za maabara, pamoja na majokufu ya kutunzia dawa, damu na chanjo.
Kituo hicho pia, Kimepataa jenerata kubwa ya kisasa inayowezesha huduma mbalimbali za matibabu kuendelea kutolewa hata pale inapotokea changamoto ya umeme kukatika.
“Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kurahisisha huduma za Afya kwa wakazi wa Mji wa Nzega. Sasa kituo hiki cha Kitengwe kimepunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya na kupunguza umbali waliosafiri na gharama na hivyo, kuokoa muda kwa wakazi hawa,” alisema Dkt. Chaduo.
Kituo cha Afya Kitengwe kwa sasa kina watumishi 18 wanaohudumia wananchi pamoja na watoa huduma za Afya ngazi ya jamii (CHW) 23, ambao hutoa huduma za awali na kusisitiza wagonjwa kufika hospitalini kwa wakati ili kuokoa maisha.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dkt. Godbless Kiguha, alisema kuwa kinahudumia wastani wa wagonjwa wa nje 30 kwa siku na wagonjwa hulazwa wastani wa wagonjwa wanane kila wiki. “Pia, takribani wagonjwa watatu hupata huduma za upasuaji kituoni hapa kila wiki, hasa wanawake wajawazito wanaojifungua,” alieleza.
Dkt. Kiguha aliongeza kuwa kituo hicho kinapata ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi. Mipango ya kujenga nyumba za makazi kwa watumishi wa afya inaendelea kwa kushirikiana na wananchi na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, Mhe. Hussein Bashe.
Kwa kuimarisha huduma, ofisi ya Mganga Mkuu imemtuma muuguzi mwandamizi kuwajengea uwezo watumishi wa kituo hicho ili kuhakikisha huduma bora kwa wakazi wa eneo hilo.
Ends