Mkuu wa wilaya ya Njombe Juma Sweda amevikabidhi hundi zenye thamani ya bil 1.8 vikundi 111 vya wajasiriamali wanawake,vijana na walemavu ambavyo vimenufaika na mikopo ya halmashauri ya asilimia 10 na kisha kuonya tabia ya kuzitumia fedha hizo kwa ulevu,mavazi na kulipa michango ya harusi.
DC Sweda amesema ili kupata tija ya mikopo hiyo vijana wajielekeze kutekeleza maandiko yao ya miradi na kisha kuhimiza kuanzisha miradi ya viwanda vya kuzalisha maji,mbegu za viazi,mazao ya misitu na parachichi na kwamba yeyote atakaeanzisha viwanda hivyo serikali itawapa eneo na kumpa fedha mapema ili kuanza utekelezaji.
” Niwapongeze wakazi wa mkoa huu hususani wakinga ambao wanaonekana bahiri kwasababu wanajua kutunza fedha ili kukuza mitaji yao ,hivyo nanyi nendeni mkatumie vyema fedha hizo”alisema Sweda.
Awali kaimu mkurugenzi Samson Meda na makamu mwenyekiti halmashauri ya mji Njombe Nestory Makenge wamesema kati ya vikundi 111 vilivyopata mikopo ,vikundi 9 vya walemavu ,39 vijana na 69 wanawake na kisha kudai kwamba hakuna upe deleo ama itikadi za kisiasa ambazo zinazingatiwa kwenye utoaji mikopo hiyo.
Kwa upande wao wanufaika akiwemo Kipson Twende mwakilishi wa kundi la walemavu wameishukuru serikali kwakuwapa fedha hizo ili kwenda kutekeleza maono yao na kwamba watarejesha kwa mijibu wa mikata yao.