Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila akizungumza na Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na viongozi hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila akisisitiza jambo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa wakati wa kikao kazi chake na viongozi hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miundombinu, Eng. Gilbert Mwoga akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila kufungua kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Msanifu Majengo Bw. Jonafrey Mwagabagu wa Idara ya Miundombinu OR-TAMISEMI akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Msanifu Majengo Bw. Jonafrey Mwagabagu wa Idara ya Miundombinu OR-TAMISEMI akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Msanifu Majengo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Chabu Nghoma akiahidi kusimamia utekelezaji wa miradi, mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila kufungua kikao kazi chao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mororogoro Mhandisi Ezron Kilamhama akieleza namna watakavyosimamia utekelezaji wa miradi, mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila kufungua kikao kazi chao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila akiwa katika kikao kazi na Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miundombinu, Eng. Gilbert Mwoga (kushoto) wakiwa katika kikao kazi na Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma.
…………..
Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Miundombinu) Mhandisi
Rogatus Mativila amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu
Miundombinu wa Sekretariati za Mikoa kuhakikisha wanasimamia
utekelezaji wa miradi kwa mujibu wa mikataba ili kuhakikisha ubora wa kazi
unafikiwa.
Mhandisi Mativila ametoa maelekezo hayo leo, wakati wa kikao kazi chake
na Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu Miundombinu, kilichofanyika katika
Ukumbi wa Kandarasi jijini Dodoma kwa lengo la kujadili kwa pamoja
mambo muhimu yanayohusiana na kazi za ujenzi, ukarabati na
matengenezo ya miundombinu katika Mikoa 26, Wilaya 139 na
Halmashauri 184 Nchini.
“Suala la ubora wa kazi ni muhimu sana, kama ni jengo lijengwe kwa
viwango vinavyostahili kwani kuna baadhi ya majengo yanatembelewa na
washemimiwa wabunge na kubainika kuwa hayana ubora,” Mhandisi
Mativila amesisitiza.
Sanjari na hilo, Mhandisi Mativila amewataka viongozi hao kuwa na
mipango ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ili waweze
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Aidha, amewataka Makatibu Tawala hao kuepuka upendeleo kwa baadhi
ya watumishi, kwani wanapompendelea mtumishi mmoja au wawili
wengine wanaona hivyo kuathiri utendaji kazi na kuongeza kuwa, iwapo
wamebaini utendaji wa mtumishi hauridhishi hawanabudi kumjulisha na
kuchukua hatua stahiki za kumjengea uwezo kiutendaji.
Mhandishi Mativila amesema, Ofisi ya Rais-TAMISEMI inatambua kazi
nzuri inayofanywa na watendaji hao, hivyo amewahimiza kuboreshe zaidi
utendaji kazi ili kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watanzania
katika maeneo ya Vijijini na Mijini.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Miundombinu Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Mororogoro Mhandisi Ezron Kilamhama amesema
kuwa, watashirikiana na wahandisi waliopo katika halmashauri ili
kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa mujibu wa mikataba na kwa
ubora unaokusudiwa.
Naye, Msanifu Majengo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Chabu
Nghoma ameahidi kuwa, watauboresha mpango kazi wao ili uweze
kutekelezeka kwa ufanisi na ndani ya mwezi huu wa pili watauwasilisha
Ofisi ya Rais-TAMISEMI ili mamlaka ione namna utakavyotekelezwa.
Ofisi ya Rais-TAMISEMI ina jukumu la kuratibu kazi za matengenezo,
ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya barabara, majengo na
miundombinu mingine katika ngazi za Mikoa, Wilaya na Mamlaka za
Serikali za Mitaa, hivyo imefanya kikao kazi hicho na viongozi hao ambao
ndio wanaisaidia ofisi kulitekeleza jukumu hilo kikamilifu.