Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipungia mkono wana CCM wakati alipowasili kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya kuongoza maelfu ya wana CCM kusherehekea miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi yanayofanyika mkoani humo kitaifa leo Februari 5, 2025.
Katika sherehe hiyo Viongozi, wanasiasa na wasanii pamoja na watu maarufu wamehudhuria katika maadhimisho hayo kama picha mbalimbali zunavyoonesha hapa chini.
NA JOHN BUKUKU -DODOMA
Mwanamuziki Diamond Platnam akitumbuiza wimbo maalum wa kumkaribisha Rais Samia Suluhu Hassan ili kuingia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 48 ya CCM.
Vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan akiingia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.