Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Arusha, Hemed Sabuni (Kulia) akikabidhi moja kati ya viti 50 kwa mkuu wa shule ya St Jude, Ndaki Saguda (wa pili kushoto), ikiwa ni moja ya jitihada za kurudisha faida kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali kwa wenye uhitaji katika maeneo tofauti nchini. Benki ya Stanbic imekabidhi viti hivyo ili kuunga mkono juhudi za Shule ya St Jude ya kutoa elimu kwa watoto wenye ufaulu mzuri na vipaji lakini wazazi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za elimu. Hafla hii ilifanyika jijini Arusha jana
Meneja wa Tawi la Benki ya Stanbic Arusha, Sabuni Hemed ( katikati ), mkuu wa shule ya The School of St Jude, Ndaki Saguda, (kulia kwake) pamoja na baadhi ya watumishi wa shule hiyo pamoja na Stanbic, wakipiga picha ya pamoja katika hafla ambayo Benki ya Stanbic ilikabidi msaada wa viti 50 kwa shule hiyo, ikiwa ni moja ya jitihada za kurudisha faida kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali kwa wenye uhitaji katika maeneo tofauti nchini. Hafla hii ilifanyika jijini Arusha jana. Shule ya St Jude inasaidia watoto wenye ufaulu mzuri na vipaji ambao wazazi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za elimu.
………………
Arusha, Jumanne, 4 Februari 2025 – Benki ya Stanbic Tanzania imeendelea kutekeleza dhamira yake ya kusaidia jamii kwa kutoa msaada wa viti 50 kwa Shule ya St. Jude iliyopo jijini Arusha. Msaada huu utawanufaisha zaidi ya wanafunzi 1,800 kutoka familia zenye uhitaji, kuwasaidia kupata elimu bora katika mazingira mazuri ya kujifunzia.
Hii ni sehemu ya sera ya uwajibikaji wa kijamii (CSR) ya benki hiyo, inayolenga kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii kwa lengo la kuimarisha ustawi wa kielimu na kijamii. Kupitia msaada huu, Benki ya Stanbic inalenga kuboresha mazingira ya kusomea, kukuza elimu bora, na kuwafikia watoto wengi zaidi wenye uhitaji.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Arusha, Meneja wa Benki ya Stanbic, Tawi la Arusha, Hemed Sabuni, alisema, “Tunaamini elimu ni msingi wa maendeleo ya jamii. Kwa msaada huu, tunatoa mchango wetu wa kuhakikisha watoto wenye uhitaji wanapata fursa ya kujifunza katika mazingira yanayowezesha mafanikio.”
Benki ya Stanbic Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia miradi mbalimbali ya kijamii, ikiwemo sekta ya elimu, kama sehemu ya juhudi zake za kujenga jamii yenye maendeleo endelevu.