Na Mwandishi Wetu, CBE
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb), amemteua Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Prof. Edda Tandi Lwoga kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kufatilia na Kuhakikisha Raia wa Kigeni Hawajihusishi na Biashara zinazopaswa kufanywa na Wazawa Kariakoo, Dar es Salaam.
Waziri Jafo ameunda kamati hiyo ikiwa ni utekelezaji wa Maagizo ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo alitaka ufanyike uchunguzi ili kuhakikisha raia wa kigeni hawajishihulishi na biashara zinazopaswa kufanywa na wenyeji.
Prof. Lwoga ataongoza kamati yenye wajumbe 15 kwa siku 30, ambapo pamoja na mambo mengine kamati hiyo inajukumu la kufatilia utoaji leseni za biashara kwa Wazawa na Wageni sambamba na kusajili Wafanyabiashara ili kuwa na kanzidata yao.
Aidha, kamati iliyoundwa inajumuisha wajumbe kutoka taasisi mbalimbali, na kwamba wajumbe wanaweza kuongezwa kutokana mahitaji ya wakati husika.