Mabigwa wa Watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Yanga Sc wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa leo Februari 1, 2025 katika Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga Sc yamefungwa na nyota wazawa, mshambuliaji Clement Francis Mzize dakika 32, kiungo Mudathir Yahya Abbas dakika 60, kiungo Muivory Coast, Pacome Zouzoua kwa mkwaju wa Penalti dakika ya 78 pamoja na mshambuliaji Mzambia Kennedy Musonda dakika ya 86.
Kwa ushindi huo, Yanga Sc imefikisha pointi 42 katika mchezo 16 na kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi, ikiizidi pointi mbili Simba SC ambayo inamchezo mmoja mkononi ambapo Februari 2, 2025 inacheza na Tabora United mjini Tabora. Kwa upande wa Kagera Sugar baada ya kipigo cha leo wanashika nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.