Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mitambo nane katu ya tisa ya kuzalisha umeme katika mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) tayari imekabidhiwa kwa Serikali baada ya kuwashwa na hivyo imebakia mashine moja tu ambayo itakuwa tayari mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
Aidha, Dkt. Biteko ametaja ongezeko la wadau ambao wako tayari kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa umeme Afrika na kupelekea Benki ya Dunia kutoa ahadi ya dola za kimarekani bilioni 22, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) dola bilioni 18.2, Benki ya Maendeleo ya Kiislamu dola bilioni 2.7, Benki ya Maendeleo ya Asia dola bilioni 1.5, Benki ya Maendeleo ya Ufaransa dola bilioni 1 na wafadhili wengine lukuki.
Dkt. Biteko ameyasema hayo Januari 31, 2025 Bungeni – Jijini Dodoma.